Idara ya wanawake kanisa la aict (taifa) yaanza semina shinyanga askofu bugota asisitiza ushirikiano

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Makamu wa Askofu Mkuu wa
AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland
Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga leo amefungua semina ya idara ya wanawake
wa AICT ambayo itafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM
mjini Shinyanga.

Askofu Bugota ametumia
nafasi hiyo kuwakumbusha kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau
wengine katika juhudi za kukemea mmomonyoko wa maadili, tabia na destori
kandamizi pamoja na migogoro ya ndoa na familia.

Amesema ipo haja ya
kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha wanapaza sauti ya pamoja kukemea tabia
zinazokwenda kinyume na maadili ikiwemo mavazi yasiyo na staha.

“Zipo
changamoto zinazohitaji mkakati wa pamoja moja wapo ya kazi kubwa ambayo idara
ya wanawake iko mbele yenu ni mmomonyoko wa maadili ambayo inahitaji mshikamano
wa pamoja katika kuishughulikia, tunaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa wito
kwa wadau kushirikiana katika kukemea matendo yanayoleta aibu kwa jamii yetu”.

“Wanawake
waumini wa kanisa la AICT tuwe mstari wa mbele kukemea na kutoa elimu za
kubadili tabia tuzikatae tabia kama za ushoga, kutoheshimiana, kuzoelea
mitandao michafu, uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi na tabia
zingine kama hizo, neno la Mungu linaagiza ‘wala msifuatishe namna ya Dunia
hii, bali mgeuzwa kwa kufanywa upya nia zenu mpate kujua kakika mapenzi ya
Mungu yalivyomema ya kupendeza na ukamilifu”.amesema Askofu Bugota

“Kuna
migogoro ya ndoa na familia hii ni mojawapo ya chanzo cha ongezeko la watoto wa
mitaani n ahata mauaji ya kutisha tunayoyaona katika jamii na kundi kubwa la
waathirika ni wanawake na watoto lakizi zipo tabia na desturi kandamizi
tuendelee kuelimisha kanisa ili waumi wetu wawe mstari wa mbele katika
mabadiliko haya”.
amesema Askofu Bugota

Askofu Bugota ametumia
nafasi hiyo kuwaomba wanawake hao kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza
ikiwemo zile za kiuchumi ili kupata vyanzo vya mapato vitakavyowawezesha
kujikwamua kimaisha.

“Zipo
rasilimali tulizopewa na Mungu tuzitumie kuboresha maisha ya watu kimsingi
mwanamke akiimarika kiuchumi familia na kanisa litaimarika pia kiuchumi tuweke jitihada
katika kulinda rasilimali zetu hii ikiwa ni pamoja na kupanda miti na kuepuka
kupanda miti ovyo lakini pia kuharibu vyanzo vya maji tuendeleze kauli mbiu ya
Tanzania Nchi ya kijani na mtu na mti”.

“Jitihada
za mafundisho ya neno la Mungu kuhusu Imani na wokovu zipewe kipaumbele katika
kutatua changamoto ya uchanga wa maisha ya kiroho lakini pia upo uchumi duni kwa
wanawake katika kanisa na jamii tuweke jitihada za makusudi za kuwasaidia
waumini kuzibaini rasilimali zilizopo na kuzitumia ili kuondokana na hali duni
ya maisha idara ya wanawake iongeze mafundisho ya ujasiliamali kwa wanawake na
kuwasaidia kuunda vikundi vya kiuchumi ili kutoa fursa kwa wanawake kupata
mikopo ya kifedha ya serikali au taasisi za kifedha”.
amesema
Askofu Bugota

Mwenyekiti wa idara ya
wanawake kanisa la AICT Bi. Martha Misoji amemshukuru Askofu Bugota ambapo
ameahidi kuwa idara hiyo itaendelea na jitihada mbalimbali za kuwaimarisha
wanawake wa kanisa hili.

Amesema Dayosisi
zinazoshiriki semina hiyo ni Dayosisi ya Pwani, Dayosisi ya Mwanza, Dayosisi ya
Geita, Mara, ukelewe pamoja na Dayosisi ya kati.

Mwenyekiti wa CCT Bi. Naila
Mayala naye ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa
mabalozi wazuri kwa wengine.

Aidha Bi. Naila amewaomba
wanawake hao kuendelea kushirikiana katika kutokomeza Mmomonyoko wa maadili na
kutoa elimu juu ya malezi na makuzi ya watoto.

Wanawake wa kanisa la
AICT katika Dayosisi saba leo Jumatano Juni 14,2023 wameanza semina ya siku
tatu yenye lengo la kuwaimarisha kimwili na kiroho kukemea mambo maovu ikiwa ni
maandalizi ya kuelekea wiki ya wanawake inayofanyika kila Mwaka mwezi Septemba.

Makamu wa Askofu Mkuu wa
AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland
Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga akifungua semina ya idara ya wanawake
katika ukumbi wa mikutano chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

Makamu wa Askofu Mkuu wa
AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland
Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga akizungumza kwenye hiyo katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa idara ya
wanawake kanisa la AICT Bi. Martha Misoji akizungumza kwenye semina hiyo leo
Jumatano Juni 14,2023 katika ukumbi wa mikutano chuo cha SHYCOM mjini
Shinyanga.

 

Semina ya idara ya
wanawake wa kanisa la AICT ikiendelea katika ukumbi wa mikutano chuo cha ualimu
SHYCOM mjini Shinyanga.