Na Jane Edward, Arusha
Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusomea kozi za uongozaji wa meli ili waweze kunufaika na fursa zote na kuweza kupata ajira kwa urahisi.
Akizungumza jijini Arusha Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI),Azan Juma Azan katika Maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayofanyika jijini Arusha.
Azan amesema kuwa, uwiano uliopo chuoni hapo kati ya wanawake na wanaume bado idadi ya wanawake ni ndogo ikilinganishwa na wanaume na hiyo ni kutokana na dhana iliyokuwepo ya kuwa kozi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu.
Amesema kuwa wamefungua dirisha la usajili kwa ngazi ya cheti hadi diploma kwa dirisha la masomo Septemba hivyo wanatoa rai kwa watu mbalimbali kujitokeze kwa wingi .
Naye Mmoja wa wanafunzi ,Wilfrida Ngallu mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika shahada ya uhandisi wa meli na vifaa vya madini,amesema kuwa,pamoja na kuwa watu wanachukulia kozi hiyo kama kozi ya wanaume peke yake lakini yeye amethubutu kusomea kwani ana shauku kubwa ya kusafiri duniani .