Dr Philip Mpango Makamo wa Rais wa Tanzania akihutubia Mkutano wa wanahisa jijini Arusha. |
Makamo wa Rais Dr Mpango akimsikiliza mjasiriamali. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya CRDB akielezea mafanikio ya Bank hiyo kwa Mgeni rasmi. |
Na Jane Edward, Arusha
Makamu wa Rais , Dk .Philip Mpango amezitaka Taasisi za fedha nchini kutoa mikopo ya riba nafuu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini,wavuvi, wakulima na wafugaji ili waweze kupiga hatua katika kiuchumi.
Akizungumza jijini Arusha wakati wa kufungua semina kwa wanahisa wa benki ya CRDB inayofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Aicc jijini Arusha.
Amesema taasisi nyingi za fedha zimekuwa zikitoa mikopo ya riba kwa asilimia 9 ,hivyo aliomba kupunguza zaidi chini ya asilimia 9 ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo na wananchi waliopo vijijini kuweza kupata huduma za mikopo yenye riba nafuu
.
Pia ameyataka mabenki kuzingatia ufanisi katika utendaji kazi ikiwemo kuongeza gharama za uendeshaji katika matumizi ya Tehama , sambamba na kuhakikisha hakuna mikopo chechefu mipya na kuzingatia ukomo wa asilimia 5 uliowekwa na benki kuu ya BOT.
Dr Ally Laay Mwenyekiti wa bodi Bank ya CRDB akizungumza katika mkutano huo. |
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB, Dk Ally Laay ameomba serikali kupitia wizara ya elimu kuandaa mitaala maalumu wa kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuwekeza katika Hisa ili kuwapa elimu ya fedha na matumizi sahihi.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwekeza kwenye hisa kwani kama Taifa kuna mwako mdogo sana ya uwekezaji katika maswala ya Hisa .
Awali Mkurugenzi wa benki ya CRDB, Abdulmajjid Nsekela amesema semina hiyo ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka wa kutoa elimu ili kuhamasisha idadi ya wanahisa ambayo ni chache kwa mabenki mbalimbali hapa nchini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha ndio maana kumekuwa na utaratibu wa kutumia semina ya wanahisa.