Askofu dkt. yohana ernest nzelu awekwa wakfu kkkt dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa victoria

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Askofu
mteule Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu leo amewekwa wakfu kuwa Askofu wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa
Victoria.

Ibada
ya kuwekwa wakfu Askofu huyo  Mch. Dkt.
Yohana Ernest Nzelu na msaidizi wa Askofu mteule Mch. Daniel Henay Mono imefanyika  katika kanisa kuu Ebenezer mjini
Shinyanga  ambapo  ibada hiyo imeongozwa na  mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo.

Akiongoza
ibada hiyo Askofu Dkt. Fredrick Shoo amemweka wakfu na kumtangaza  Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa Askofu wa
KKKT Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Victoria.

‘Natangaza mbele ya umati huu wa mashahidi kuwa leo
kuanzia siku hii ya Bwana ya tatu baada ya Pasaka tarehe ya 30 ya Mwezi Aprili
Mwaka huu 2023 wewe Mchungaji Dkt. Yohana Ernest Nzelu umekuwa Askofu wa Kanisa
la Mungu katika jina la Baba nala Mwana nala Roho mtakatifu nenda sasa
ukatumike kama Bwana alivyopenda kukutumia Amina’

Akizungumza
baada ya kuwekwa wakfu Askofu huyo ameahidi kutoa ushirikiano katika huduma za
Dini pamoja na hudumza kijamii na kwamba amewapongeza viongozi wa serikali kwa
ushirikiano wao na viongozi wa Dini huku akiwaomba kuendelea kushirikiana siku
zote.

Askofu
Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu wakati akizungumza kwenye ibada hiyo ametaja  baadhi ya changamoto zinazokwamisha huduma za Kanisa
pamoja na changamoto za wananchi hasa katika Mkoa wa Shinyanga.

‘Bado kunauhitaji mkubwa wa barabara za mitaa katika
Wilaya ya Kahama na pia kumalizia kipande cha Old Shinyanga hadi Bubiki, kuna
changamoto juu ya ujenzi wa ukarabati wa uwanja wa Ndege wakazi wa mikoa hii
miwili Shinyanga na Simiyu wanapata adha kubwa sana ya kuunganishwa na maeneo
mengine kwa njia ya anga ombi langu kwa serikali kwa mara nyingine tene
iangalie mchakato huu uweze kukamilika’

‘Tunatiwa moyo sana na miradi ya kimkakati inavyoshughulikia
tunaona kazi zinaendelea na tunaona kazi za bomba la mafuta tunaomba sana ajira
zizingatiwa wazawa wenye ujunzi wa eneo husika’

‘Kuna umakini unahitajika sana kwetu sote hasa juu ya
kukaribisha asasi zisizo za kiserikali kwa habari tunazoziona mitaani na
kuzisikia hili swala la ushoga ni janga linalotakiwa kupigwa vita sana katika
Nchi yetu hili ni chukizo mbele za Mungu   tunatamani kusikia sauti kali ya serikali
dhidi ya jambo hili sisi kama Kanisa kwa nafasi yetu tunaahidi kutoa ushirikiano
katika kupigana vita hii na Mungu atusaidie’

Akitoa
salam za serikali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme amesema
serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa Dini na  kushughulikia changamoto zilizopo katika Mkoa
wa Shinyanga

‘Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za  Dini ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu,
katika changamoto zilizotajwa ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara
Wilaya ya Kahama napenda kuwataarifu kuwa serikali imeanzisha mradi
unaojulikana kama Taktiki ambao unalenga kuboresha miundombinu miji 45 za
Tanzania zikiwemo Manispaa zetu mbili za Wilaya ya Kahama na Shinyanga mjini
kupitia mradi huu Manispaa ya Kahama itajenga kil. 24. 2 kwa kiwango cha lami
lakini pia itajenga stendi kuu ya mabasi cha kisasa na soko kuu la kisasa’

‘Ujenzi wa kiwanja cha Ndege katika eneo la Ibadakuli
Shinyanga napenda kuwataarifu kuwa utekelezaji wa ujenzi umeanza kwa Ghalama ya
Shilingi Bilioni 52 na Milioni 868 Mheshimiwa Rais tayari amekwisha zitoa fedha
hizi mkandarasi tayari amekabidhiwa eneo la mradi na utekelezaji wake
unakamilika ndani ya Miezi mitatu, changamoto zingine za ujenzi na ukarabati wa
barabara Mkoa wa Shinyanga  tayari
serikali yetu imeanza kuzifanyia kazi’

RC
Mndeme amewakumbusha wakristo kuzingatia misingi ya Dini huku akiwasihi
viongozi wa Dini kushirikiana ili kutokomeza mmomonyoko wa maadili katika jamii
na Taifa kwa ujumla.

‘Tuendelee kuheshimu imani yetu pia wazazi na wananchi
tuendelee kuwalinda watoto wetu dhidi ya ukatili wanaofanyiwa tukemee matendo yasiyofaa
kwa vitendo tuziishi amri 10 tulizopewa na mwenyezi Mungu na sisi serikali
hatuyabariki mambo yanayoenda kinyume na tamaduni zetu viongozi wa Dini,
serikali na jamii nzima tuungane kwa pamoja kusimamia maadili ya watoto wetu,
amesema RC Mhe. Mndeme

Askofu
Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu leo Jumapili Arili 30, 2023 amewekwa wakfu kuwa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Victoria ambapo ibada hiyo
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na serikali huku mgeni rasmi akiwa
mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkuu
wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo akizungumza kwenye ibada ya kuwekwa wakfu
Askofu mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu na msaidizi wake Mch. Daniel Mono katika
Kanisa kuu la Ebenezer mjini Shinyanga.

Askofu
Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu wa kanisa kuu Ebenezer akizungumza baada ya
kuwekwa wakfu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.. Christina Mndeme akitoa salam za
serikali kwenye ibada hiyo.

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo
Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo
Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 

Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu kuwa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea leo
Jumapili Aprili 30,2023 katika Kanisa kuu Ebenezer mjini Shinyanga. 








Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa
wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest
Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.

Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa
wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest
Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.

Awali yakifanyika maandamano kuelekea kwenye Ibada ya kuwekwa
wakfu  Askofu Mch. Dkt. Yohana Ernest
Nzelu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria  leo Jumapili Aprili 30,2023.