Ruwasa shinyanga yakabidhi mtambo wa kisasa wa kuchimba visima vya maji, rc mndeme ataka wananchi kutunza miundombinu

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Serikali ya Mkoa wa
Shinyanga imepokea mtambo wa kisasa utakaotumika kuchimba visima vya maji, kwa
fedha za mradi wa  Uviko 19 ambao
utawanufaisha wananchi  katika Wilaya ya
Kishapu pamoja na Halmashauri ya Ushetu.

Katika taarifa yake
wakati akikabidhi mtambo huo, Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira
vijijini RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amesema Mkoa wa
Shinyanga ni moja ya Mikoa inayokabiliwa na ukame kutokana na sababu mbalimbali.

Mhandisi Payovela
ameeleza kuwa Mkoa wa Shinyanga pamoja na kunufaika na mradi wa maji ya ziwa
Victoria lakini bado yapo baadhi ya maeneo yenye changamoto ya maji ambapo ili
kutatua changamoto hiyo serikali 
imenunua mitambo 25 itakayotumika kuchimba mabwawa ya maji.

“Mkoa
wa Shinyanga ni moja ya mikoa kame (semi – arid Region ), kutokana na hali hiyo
upatikanaji wa vyanzo vya maji chini ya ardhi imekuwa changamoto hata hivyo
Mkoa wa Shinyanga ni mnufaika wa kwanza wa mradi wa maji ya ziwa Victoria ambao
kwa sasa unahudumia mikoa ya Mwanza (Kwimba na Misungwi), Shinyanga, Tabora
(Igunga, Tabora na Nzega) na mji wa Shelui Mkoa wa Singida”.
amesema
Mhandisi Julieth Payovela

“Ujenzi
wa miradi ya maji kupitia bomba kuu la KASHWASA umeendelea hadi sasa jumla ya
vijiji 89 vinapata maji na vijiji 50 ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji
kupitia bomba hilo upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji”.

“Uunganishaji
wa maji ya KASHWASA umeendelea kufanyika kwa vijiji vilivyondani ya umbali wa
km 12 kutoka bomba kuu la KASHWASA katika vijiji vilivyombali zaidi na mtambo
wa KASHWASA tumeendelea kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa
visima virefu”.
amesema Mhandisi Julieth Payovela

Meneja huyo wa RUWASA
Mkoa wa Shinyanga amesema Mhandisi Julieth Payovela ametaja Wilaya
zitakazonufaika na  uchimbaji visima
katika Mkoa wa Shinyanga kuwa ni kishapu na kahama katika halmashauri ya
Ushetu.

“Serikali
ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan imenunua mitambo 25 na seti 5 ya kuchimba mabwawa  ya maji iliyonunuliwa na Rais Dkt. Samia
kupitia wizara ya maji kwa fedha za Uviko – 19, mtambo huu ambao tumeukabidhi
leo ni moja ya mitambo iliyonunuliwa kwa ajili ya uchimbaji wa visima mtambo
huu unauwezo wa kuchimba kisima hadi mita 300”.
amesema
Mhandisi Julieth Payovela

“Aidha
kupitia fedha za Uviko 19 Mkoa wa Shinyanga ulitekeleza miradi ya maji, mradi
mmoja kila jimbo isipokuwa jimbo la Solwa imejengwa miradi miwili jumla ya
fedha kiasi cha Tsh. 3061,459,641.73 zimetumika kutekeleza miradi saba (7)
miradi yote imekamilika na wananchi 26,902 wanapata huduma”.

“Mtambo
huu tunaoukabidhi kwa kuanza na uchimbaji utaanza katika vijiji vinne (4)
kijiji cha Itilima na Mwashinongela vya Wilaya ya Kishapu na Ubagwe na
Kinamapula vya Halmashauri ya Ushetu”.
amesema Mhandisi Julieth
Payovela

Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mtambo huo wa maji ambao
utasaidia kutatua kero kwa wananchi.

RC Mndeme amewaomba
RUWASA kusimamia na kutekeleza  mradi huo
kwa kuhakikisha unaleta matokeo chanya kama ulivyokusudiwa huku akiwaomba
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga hasa watakaofikiwa kutunza miundombinu ya mtambo
huo.

“Niwaombe
RUWASA mtambo huu ukatumike kwa malengo yaliyokusudiwa lakini kabla ya kuchimba
kisima tuhakikishe tunafanya uchunguzi wa kina ili kujua tunapochimba kweli
maji yapo kuliko tutumie gharama kupeleka mtambo kwenda kuchimba maji kumbe
maji hamna”.

“Vile
vile niwaomba wananchi kwa pamoja tutunze miundombinu ambayo itawekwa ya maji
katika maeneo yetu na vile vile tutunze mazingira ili tunufaike sisi na vizazi
vijazo”.
amesema RC Mndeme

Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira
vijijini RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela  akisoma taarifa yake wakati wa hafla ya
kukabidhi mtambo huo.

 Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira
vijijini RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela  
akisoma taarifa yake wakati wa hafla ya
kukabidhi mtambo huo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Christina Mndeme akizungumza katika hafla hiyo

Wa kwanza upande wa kushoto ni Kaimu Meneja wa
KASHWASA, John Zengo akifuatiwa na 
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela, Aliyevaa suti
nyeusi wa pili kutoka upande wa kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akikata utepe kwenye hafla hiyo na wa kwanza upande wa kulia
ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mhandisi Yusuph Katopola.