Serikali yafanikiwa kudhibiti ugonjwa wa marburg ulioripotiwa kagera

Na
Mapuli Misalaba

Serikali
imefanikiwa kudhibiti ugonjwa wa  MARBURG
ulioripotiwa katika Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kuwa jumla ya watu nane (8) walithibitika ambapo watano (5) kati
yao walifariki na watatu (3) wanaendelea na matibabu
katika vituo vya
kutolea huduma.

 Taarifa hiyo
imetolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu hii
 March 25, 2023 wakati akizungumza na Waandishi
wa Habari katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kusema mpaka sasa hakuna
visa vipya vya wagonjwa wala kifo kilichotokea.

 Waziri Ummy Mwalimu
 amesema kuwa serikali imefanikiwa
kudhibiti ugonjwa huo usisambae maeneo mengine Nchini na kwamba mpaka sasa
jumla ya watu 205 wanafuatiliwa kwa karibu kwa kuwa
walitangamana na wagonjwa au wahisiwa.

 “Niwatoe hofu wananchi
kuwa Serikali imeudhibiti ugonjwa huu usisambae maeneo mengine nchini hadi sasa
kama tulivyoeleza hatujapata wagonjwa au wahisiwa wengine nje ya kaya mbili
zilizoripoti awali ambazo ni kata ya Maruku na Kanyangereko”.
amesema Waziri Ummy

 “Hadi kufikia  tarehe 25 Machi, 2023, tumeendelea kushuhudia
kwamba ugonjwa huu unadhibitiwa maana hatujapata wagonjwa wapya waliothibitika,
licha ya kuendelea kupokea tetesi na wahisiwa kadhaa. Mfano, siku ya tarehe 22
Machi, 2023 tulipata wahisiwa watatu (3) na wote baada ya kuchukuliwa sampuli,
wamekutwa hawana maambukizi.

 “Tumeongeza wataalam 6
wa afya ikiwemo daktari bingwa bobezi wa magonjwa ya Figo, daktari bingwa wa
magonjwa ya ndani na wauguzi waliopata mafunzo maalumu kutoka maeneo mengine
ili kusaidiana na wataalam wa Afya wa hapa Mkoani Kagera katika kuendela kutoa
huduma kwa wagonjwa watatu waliopo katika vituo vyetu vilivyoandaliwa”.
Amesema Ummy

 “Lakini tunaendelea kufuatilia
watu waliotangamana kwa namna mbalimbali na wagonjwa au wahisiwa, ambapo hadi
leo tuna jumla ya watu 205
tunaowafuatilia (contacts) kwa karibu kwa kuwa walitangamana na wagonjwa au wahisiwa
watu hawa wote ni wanafamilia waliouguza wagonjwa na watumishi wa Afya
waliohudumia wagonjwa watu hawa kwa mujibu wa taratibu za afya kuhusu udhibiti
wa maambukizi, tunawafuatilia kuhusu mwenendo wa afya zao kwa kipindi cha siku 21 ili kujiridhisha
endapo wataonyesha dalili za ugonjwa au la”.
amesema Waziri wa Afya Mhe. Ummy

 Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu amefafanua namna ugonjwa huo unavyoambikizwa ikiwemo
mkojo, damu, machozi, kutoka kwa wanyama, pamoja na kugusa majimaji ya mwili wa
mtu mwenye ugonjwa huo.

 “ Ugonjwa wa Marburg
huambukizwa kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine hususan kwa njia ya
kugusa majimaji mfano mate, mkojo, damu, machozi au kinyesi kutoka kwa mtu
aliyefariki kwa ugonjwa huu au kutoka kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya
Marburg anayeonyesha dalili za ugonjwa huu vilevile, maambukizi yanaweza pia
kutokea kutoka kwa wanyama hasa Popo, Tumbili na  Nyani na kwenda kwa binadamu iwapo mtu
atakula au kugusa mizoga au wanyama walioambukizwa”.

 “Serikali pia
imeimarisha ufuatiliaji wa visa na wahisiwa katika jamii yetu yote kwenye
maeneo hatarishi ikiwemo visiwa vya Ziwa Victoria  ili kujihakikishia kuwa tunaendelea kuwa
salama. Aidha tunaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu ugonjwa huu ikiwemo dalili
na jinsi ya kujikinga”.
amesema Mhe. Ummy

 “Timu za wataalam wetu
wako maeneo mbalimbali ikiwemo pamoja na mipaka yetu ili kuimarisha zaidi
udhibiti wa ugonjwa huu. Niwaombe ndugu zangu wana Bukoba na wanaKagera kwa
ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zaidi zitakazosaidia kuudhibiti
ugonjwa kwa haraka zaidi”. Amesema Ummy Mwalimu

 Aidha Waziri huyo ametumia nafasi hiyo
kuwaomba wananchi wote kuendelea kuzingatia Miongozo na Taratibu za Kuzuia na
Kudhibiti Maambuzi zinazotolewa na wataalam wa Afya ikiwa ni pamoja na kutoa
taarifa za ugonjwa huo kwa wakati.

 “Nawaomba muendelee
kuzingatia Miongozo na Taratibu za Kuzuia na Kudhibiti Maambuzi (Infection
Prevetion and Control) wakati wote wa kutoa huduma kwa wagonjwa ni matumaini
yangu kwamba ugonjwa wowote wa kuambukiza hautawakuta kwa kuwashtukiza bali
mtaubaini mapema na kuuzuia katika eneo moja na kutoa tiba stahiki”.

 “Hata hivyo nawaomba
wananchi wote kuendelea kuzingatia njia za kujikinga na tahadhari dhidi ya
ugonjwa huu aidha ninawaomba wananchi 
kote nchini kufuatilia taarifa rasmi za mwenendo wa ugonjwa huu kutoka
Wizara ya Afya na Mamlaka husika za Serikali sambamba na kutoa taarifa kwa
Serikali kupitia Ofisi za Serikali za Vijij/Mitaa au Vitongoji  au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo
kuna mtu mwenye dalili zinazofanana na ugonjwa huu”.
amesema Ummy

 Serikali
kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Kagera na Wadau mbalimbali inaendelea kudhibiti
  maambukizi ya ugonjwa huu kwa kutekeleza
mikakati mbalimbali ikiwemo uimarishwaji wa elimu ya afya kwa umma na
ushirikishwaji wa jamii, ufuatiliaji wa wagonjwa na wahisiwa, afua ya udhibiti
wa magonjwa ambukizi yaani
Infection
Prevention and Control
  sambamba na
huduma za upimaji na tiba dhidi ya ugonjwa wa Marburg.

    Siku
kumi (10) zimepita tangu tupate taarifa za ugonjwa wa Marburg katika kata za
Maruku na Kanyangereko, Halmashauri ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera ambapo tarehe
21 Machi 2023 Waziri wa Afya Mhe. Ummy alitangaza rasmi kuhusu uwepo wa
maambukizi ya Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Marburg baada ya majibu ya
uchunguzi wa kimaabara kuthibitisha uwepo wa Virusi hivyo.
 

 Mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Marburg
hawezi kuambukiza wengine kabla hajaonesha dalili za ugonjwa huu”.