Wasichana 7000 kunufaika katika mradi wa bilioni45

Washiriki wa mkutano wakiwa katika picha ya pamoja
Mshauri wa mradi Dkt Alice Mumbi

Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Wanawake na Wasichana zaidi ya 7000 kutoka katika wilaya 7 nchini walioshindwa kuhitimu masomo yao kwa sababu mbalimbali wanatarajiwa kunufaika na mradi wa ubia wa uwezeshaji kupitia ujuzi(ESP) .

Mradi huo utakaodumu kwa miaka7 unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania,  utagharimu Bilioni 45 hadi utakapokamilika.

Akiongea jana jiji hapa mshauri wa masuala ya jinsia ambaye pia ni mshauri wa mradi huo, Dkt  Alice Mumbi amesema kuwa mradi huo utaweza kuwasaidia watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuwagawia vifaa.

Alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika halmashauri 7 ambazo ni Monduli, Morogoro, Kilwa, Singida, Nzega, Kasulu, Tarime, Kondoa, na Njombe.

“Siku ya Leo tumekutana hapa jijini Arusha, tunalenga kuwainua watoto wa kike na tunarajia matokeo ya mwisho ya ESP ni kuboresha ushiriki wa wanawake na wasichana kiuchumi nchini Tanzania”aliongeza

Amesema ndani ya mradi huo pia jumla ya wanafunzi 3200 wataweza kushiriki katika shughuli za usawa wa kijinsia na uhamasishaji wa haki za  binadamu, huku jumla ya wafanyakazi 180 wataweza kufunzwa ujuzi wa kiufundi na ufundishwaji na kutoa moduli za usawa wa kijinsia na haki za binadamu.

Awali katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia, Dkt.Francis Maiko amewataka wasichana na wanawake kuchangamkia fursa hiyo ili kujikwamua kiuchumi.

Amesema vyuo vya maendeleo ya wananchi vimekuwa taasisi za misingi za kudahili wanafunzi na makundi ya watu waliopo pembezoni ambao  wamekuwa wakiacha masomo kutokana na sababu mbalimbali za kimazingira.<

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Maiko akitoa hotuba ya ufunguzi katika mkutano huo

Amesema hayo yote ndio yamesababisha wataalamu na wadau ambao watafanya kazi katika mradi huo kukutana kwa lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na kuwaondolea  vikwazo vya ajira.