Waziri mkuu afungua mkutano wa kimataifa wa utalii, wadau waanza kujadili janga la uviko19

 Na Queen Lema Arusha

Waziri mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kassimu Majaliwa  amefungua mkutano  wa Mawaziri wa utalii kutoka zaidi ya nchi 50 wanachama wa shirika la utalii Duniani na maafisa wa Kamisheni  ya Afrika  

Aidha mkutano huo ambao umefunguliwa jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya utalii umeweza kujadili hali ya utalii baada ya janga la Covid 19

Akifungua mkutano huo, Waziri Majaliwa alifafanua kuwa serikali inaendelea kufanya mikakati mbalimbali ya  kuboresha utalii 

“Mnamo Mwaka 2019 kabla ya mlipuko wa janga la Uviko 19 mapato yatokanayo na sekta ya utalii kwa Tanzania yalifikia dola za kimarekani Bilioni 2.9 na kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja milioni 2.5,” alisema.

“Na katika kipindi hicho sekta ya utalii ilichangia wastani wa asilimia 17.2 ya pato ghafi la taifa,” aliongeza.

Aidha waziri huyo Mkuu aliwataka washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inaendelea kuongeza nguvu katika kulinda na kuhifadhi utalii wa rasilimali za asili na kuhakikisha unaendelea kuwanufaisha wananchi wa nchi hiyo na taifa kwa ujumla

“Hatua hii ni kielelezo tosha cha matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jumuiya za kimataifa ikiwemo shirika la utali duniania hasa katika kuendelea sekta muhimu ya Utalii pamoja na masuala ya uhifadhi,” alisema.

Kwa upande wake katibu wa shirika la utalii Duniani kamisheni ya Afrika Bw Zurab Pololikashvili alisema pamoja na changamoto zilizopo bado kuna umuhimu wa kuendelea na utalii na akaipongeza Tanzania kwa kuendelea kuimarisha misingi ya uhifadhi na utalii.

“Nafurahi na kufarijika kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, nchi ambayo inasifika kwa kitovu cha utali duniania ,baada ya janga la kovidi wakati sasa umefika wa kuinu sekta hii na kuhakikisha inasaidia masuala ya kiuchumi na kijamii,” alisema.

Shirika la utalii duniani ambalo kwa sasa makao yake makuu yako Uhispania Lilianzishwa mwaka 1946 mjini London, nchini Uingereza na Tanzania ilijiunga na shirika hilo mwaka 1975.