Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Profesa Godius Kahyarara akizungumza na wajasiliamali hawapo pichani katika siku ya Nssf Day kupitia maonyesho ya madini yanayoendelea mkoani Geita |
Na Mwandishi Wetu, Geita
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Geita Profesa Godius Kahyarara amewahamasisha wanachimbaji wadogo wa Madini mkoani humo kujiunga na mafuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kujiwekea akiba ya sasa na ya baadae.
Kahyarara ameyasema haya Oktoba 5 mwaka huu Kwenye Maonyesho ya tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani humo alipokuwa akizungumza na wajasiliamali pamoja taasisi za kifedha kupitia siku maalumu ya Nssf DAY yenye lengo la kutoa elimu kwa wajasiliamali hao na wachimbaji wa madini.
Amesema kuwa ni vizuri makundi ya wachimbaji wadogo pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanajiunga katika mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii jambo ambalo litawapa faida ya kuweka akiba kwa maisha ya baadae.
“Nawapongeza Nssf kwa kuja na utaratibu huu wa kutoa elimu kwa wajasiliamali na hasa yenye lengo la kuwakumbusha umuhimu wa mifuko ya hifadha ya jamii,hivyo sisi kama mkoa tumeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha tunawajengea uwezo katika shughuli zenu mnazozifanya na kubwa nijiunga na mifuko ya hifadhi hususani Nssf Kwa ajili ya akiba ya uzeeni.”amesema Professa Kahyarara
Kwaupade wake Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma (NSSF) Lulu Menegele akizungumzia siku ya Nssf kupitia maonyesho ya Madini amesema kuwa lengo la siku hiyo nikuendelea kuongeza uelewa kwa wanachama na wachimbaji wadogo wamadinini kujiunga na mfuko wa hifadhi ya Taifa ya Jamii Nssf.
Amesema kuwa wametumia fursa ya maonyesho hayo kutoa elimu juu ya mfuko wa jamii na kuelezea umuhimu wa namna ya kujiunga na mfuko huo nakwamba leo ni kijana na kesho ni mzee hivyo ukijiwekea akiba ya baadae na ili mwanachama awe hai lazima achangie
“Tumewafikia wananchi wa mkoa wa Geita ambapo wachimbaji asilimia kubwa sehemu ya wanachama wa mfuko wa hifadhi ya Jamii na kuhusu huduma zao wanazitoa kwa njia ya mbalimbali ikiwamo nji ya simu ya kiganjani na hata simu ndogo unaweza kutumia kujiunga na Nssf.”amesema Lulu
Pia ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Geita kujiunga na mfuko huyo na huduma hizo zinapatikana kwenye ofisi zote na mfuko zilizopo nchi nzima huku akiwasihi kuendelea kuzungukia kwenye banda lao ili kuendelea kupata elimu zaidi ya mfuko wa Nssf.
Kwaupande wake Meneja wa Nssf mkoa wa Geita Winniel Lusingu Amesema kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nssf hususani mkoa wa Geita unaendelea kuwahimiza wananchi kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa kuwa unafaida kubwa katika maisha.
Ameongeza kuwa kupitia maonyesho ya Madini wanaendelea kuandikisha wanachama wapya kwa gharama ya shilingi 20,000 huku wakizingatia kauli mbiu ya ”huduma bora kipaumbele chetu”
“Mfuko wa Hifadhi wa Jamii Nssf Mkoa wa Geita tunaandikisha wanachama lakini kisha tunapinga rushwa kwa nguvu zote na katika hili nawaomba wanachama wetu kufika kwenye banda letu lililopo hapa kwenye viwanja vya maonyesho na ofisi zetu zilizopo hapa Geita ili kupata huduma zetu.”amesema lussingu
Kwa upande wake Meneja wa Sekta isiyo rasmi NSSF Makao Makuu Rehema Chuma amesema kuwa Nssf Inafikia makundi mbalimbali ya wajasiliamali likiwemo kundi kubwa la wachimbaji wadogo la madini ya dhahabu kuwapa elimu na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika nakuona shughuli ya uchimbaji ina tija.
Pia Rehema amewahamiza wajasiliamali hao hususani wanachama kujishughulisha na shughuli itakayomuwezesha kuchangia mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nssf ili baadae ayaone manufaa lakini pia akiwa na mchango wake kwenye mfuko anaweza kukopesheka na taasisi mbalimbali za kifedha.
“Ndugu zangu wajasiliamali na wanachama wa mfuko huu huduma nyingine ambayo mnanufaika nayo ni mafao ya walemavu,wajawazito,na wenye matatizo mbalimbali wananufaika na mafao haya hivyo nawaasa kuchangamkia fursa hii muhimu na pia kuwekeza Nssf kwa ajili ya Malengo yenu ya baadae kwani masikini wa leo ni utajiri kesho..”amesema Rehema
Pia katika warsha hiyo amesisitiza makundi mbalimbali kuendelea kujiunga mfuko huo ili kujijengea maisha ya sasa na ya baadaye huku baadhi ya mnufaika wa mfuko huo Christopher Gonya alipata fursa ya kuzungumzia mafanikio yake kupitia mfuko huo nakuhamisha wengine kujiunga nao.