Naibu katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo akipata maelezo kutoka katika banda la GF Truck, katika maonyesho ya madini Geita |
Naibu Katibu Mkuu wizara Madini Msafiri Mbibo avutiwa na banda la Gf Truck Group,maonyesho ya madini geita.
Na David John Geita
NAIBU Katibu mkuu wa Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ametembelea Banda la Gf Truck Group lililopo kwenye maonyesho ya tano ya madini yanayoendelea mkoani Geita huku akisifu namna kampuni hiyo ilivyojipanga katika kusaidia wachimbaji wadogo.
Akiwa katika banda hilo Naibu katibu mkuu huyo Mbibo alipata fursa ya kupata maeleze kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Smart Deus pamoja na Meneja Mauzo Paul Msuku juu ya ushiriki wao kwenye maonyesho hayo na namna walivyojipanga katika kufikisha huduma zao kwa jamii hususani wachimbaji wa madini.
Akitoa maelezo hayo leo Septemba 28 mwaka huu Meneja mawasiliano huyo,Deus amesema kuwa wao kama kampuni,moja ya huduma ambazo wanazitoa ni pamoja na kuwapa unafuu wachimbaji wadogo wadogo na wakati wa madini kwa kununua mashine na gari kwa malipo ya kidogo kidogo huku wakitanguliza nusu kama malipo ya awali.
“Ndugu katibu mkuu karibu kwenye banda letu la GF Truck Group kama unavyoona tupo kwenye maonyesho haya ya tano ya madini na sisi kama kampuni Gf Truck ni moja ya wadhamini wakuu wa maonyesho haya na tumekuja kuwapa huduma wananchi hususani wachimbaji na tumekuja na gari pamoja na mashine aina ya Excavator Xe 215c kwaajili ya shughuli za uchambaji madini.”amesema Deus
Nakuongeza kuwa kampuni ya Gf Truck Group kwa kutambua umuhimu wa maonyesho haya tunashiriki katika shughuli za kijamii kama vile kutoa damu na kutoa zawadi mbalimbali kwa washiriki ikiwa ni sehemu moja wapo ya kurudisha kwa jamii kinachozalishwa.”amesema Deus
Deus ametumia fursa hiyo kuwaomba wa kazi wa mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi siku ya ocktoba 1 mwaka huu ili kuweza kuchangia damu kwa ajili ya watanzania wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wamelezwa hospitali na wanamahitaji makubwa ya huduma ya damu.