Na Veronica Mheta, Arusha
TANZANIA kuwa mwenyekiti wa mkutano wa tatu wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozalisha Almasi Afrika (ADBA) ambao utaidhinisha katiba,kanuni na miongozo ya umoja huo
Mkutano huo unaoendela leo Jijini Arusha utateua viongozi watatu wa sekretarieti ambao ni katibu Mtendaji na manaibu wake wawili.
Waziri wa Madini ,Doto Biteko,amesema mkutano huo wa tatu wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya nchi za Afrika zinazozalisha Almasi (ADPA) kwa mujibu wa utaratibu ulianza Aprili 7 mwaka 2022 kwa kamati ya wataalamu kuchambua na kujadili nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mapitio na marekebisho ya nyaraka zinazosimamia ADPA
Biteko anasema lengo kubwa la kuunda ADPA ni kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika Jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama.
“Tanzania ilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la ADPA mwaka 2021 kwa kipindi cha miaka miwili,hivyo tunatarajia kukabidhi uenyekiti wetu kwa Jamuhuri ya Zimbabwe Machi mwaka 2023”
Amesema katika kipindi cha Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, imekuwa ni heshima kubwa kwao kwa kuwajibika, kwa ajili ya kuwezesha maendeleo ya nchi zao hususan katika usimamizi wa madini ya almasi