Na Mwandishi wetu
MKAZI wa kijiji cha Nagulo kilichopo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Bibi Pelis Nyanyihindi (78)amesikitishwa na kitendo cha kutishiwa maisha na baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao walivamia shambani kwake juni 13 mwaka huu na kuaza kufyeka pasipokuwa na kibari chake.
Akizungumza na waandishi wa habari ambao walisafiri kutoka Dar Es Salaam hadi kijijini hapo Bibi Pelis Nyanyihindi amesema kuwa shamba hilo ambalo ni hekari 14 analimiliki tangu ujana wake hivyo alishangazwa na hatua ya vijana hao ambao hakuwataja majina yao kuvamia na kuaza kufyeka huku wakimtishia maisha kwa kumtaka kutosema chochote.
Bibi Pelis amefafanua kuwa awali shamba hilo lilikuwa na kesi na mmoja wa mjukuu wake ambaye alitaka kumnyang’anya hatua ambayo iliwafanya kufikishana hadi Baraza la kijiji, kata na baadae Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Chamwino ambapo Juni 9 mwaka huu huku ilitoka na Bibi Pelisi alipewa haki yake.
“Ndugu zangu waandishi kwakweli sina amani kabisa na hawa vijana kwani wamekuwa wakinitishia amani sana lakini nimesharipoti licha jambo hili Polisi kituo kikubwa cha Dodoma na wao wamenirudisha wilayani, naamini wanalishughulikia na vijana hawa walishakamatwa na kuwekwa lumande ila wapo nje kwa dhamana.”Amesema Bibi Pelis
Ameongeza “kuja kijana ambaye ni mjukuu wa mume wangu kwani kabla yangu alikuwa ameoa mwanamke hivyo huyo ni mkuu,anashida anataka kunidhulumu shamba langu huku akijuwa kabisa shamba hili ni la kwangu nililipata kabla ya hata kuwa na babu yake na yeye analijua hilo nashangaa anataka kunipora licha ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria na mimi kushinda lakini ananisumbua ,naamini yeye ndio alituma hata hao vijana kufyeka bila ruhusa yangu.”amesema Bibi Pelis
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Nagulo Meshack Matonya amesema kuwa ni kweli bibi huyo amekuwa akitishiwa maisha na vijana ambao walivamia shamba lake lakini kwa bahati nzuri jambo hilo lipo mikononi wa vyombo vya usalama wanaendelea kulifanyia kazi na yeye kama Mwenyekiti ataendelea kuwa karibu na Bibi huyo na yupo tayari kusimamanaye popote atakapohitajika.
‘Ilikuwa Juni 13 mwaka huu ndio vijana hao walivamia kwenye shamba la Bibi huyu na huko nyuma walifikishana hadi kwenye sheria na Bibi Pelis alishinda japo hukumu yenyewe imetolewa kwa kingereza na hapa nishauri kuwa nivema wezetu wasomi wakatoa hukumu hizi kwa kiswahili ili kutoa fursa kwa wananchi kujua kilichoandikwa kwenye hukumu.”amesemaMwenyekiti Matonya.