Wananchi wa kia (w)hai mkoani kilimanjaro wamuomba rais samia kuingilia kati mgogoro uliopo baina yao na kadco

 

Diwani wa Kata Kia Tehera Mollel,akizungumza katika mkutano wa serikali ya kijiji ulioitwa kwajili ya kujadili changamoto mbalimbali wanazozipitia ma namna ya kuzipatia ufumbuzi.

 Wakwanza kushoto ni mama Naishie Mollel ambaye mwenyeji wa Kata ya Kia Akiwa katika mkutano wa serikali ya Kijiji,kata ya KIA wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro

Katika picha ni baadhi ya wakina mama wa jamii ya kimaasai wakiwa katika mkutano wa kijiji katika kata ya KIA

Mwenyekiti wa kijiji akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katikakata ya Kia

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kia wakiwa katika mkutano wa kijiji ulioitishwa kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipitia na namna ya kuzipatia ufumbuzi
Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro
 
Wakazi wa Kijiji cha sanya stesheni ,kata ya kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kutatua mgogoro kati yao na KADCO, kwani wamekuwa na wakati mgumu ambao wanashindwa kuendelea kufanya shughuli za maendeleo kwaajili yao na watoto wao.

Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa Kata Kia Tehera Mollel,amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu , na usipotatuliwa zaidi ya wakazi 5000 wanakosa makazi kutokana na eneo hilo ,kwani hadi sasa wameshindwa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na kutangaziwa kusitisha shughuli zote haswa za ujenzi.

Mollel asema hadi sasa vijiji 7 vimeingia  kwenye mgogoro ambavyo ni vijiji vitatu kutoka kata ya Kia, mtakuja, Sanya stesheni,vingine ni  Chemka kilichopo kata ya tindigani,kata ya Arumeru ni Kijiji cha Malula,samaria na majengo ,hivyo kwa umuhimu wa uwanja wa ndege wa KIA wamemuomba Rais kwenda kutengeneze mazingira mazuri kwa wananchi wake watendewe haki ili wasiwe na wasiwasi kwenye maeneo yao.

‘’Hawa watu unaowaona haopa ni watu ambao kwenye maisha yao hawajui wataenda wapi tangia waambiwe kwamba wasijiguse tena kujenga nyumba wala nini,kwakweli jamii yote inashangaa na isitoshe kila siku vijana wanakua na wanahitaji kujenga,hivyo sisi kama jamii hii kwa taarifa hizo tunaona kabisa wanatumaliza kimaisha’’ Alisema Diwani wa Kata ya Kia.

Amesema kuwa Uwanja wa KIA una manufaa makubwa kwa Taifa na kwa halmashauri,ambapo  kata hiyo hawapingani nao,ila swala kubwa kwao wameiomba serikali kwenda kuwaangalia wananchi , kwani imekuwa kama mwiba maishani mwao, hivyo wanamuomba Mhe.Rais kwenda na kuona changamoto iliyoppo ili aweze kuwatatulia

‘’Tunaomba tume iliyokuja kuangalia na kutengeneza waraka 2006 ilitengeneza,tukiwa ndani ya mgogoro ,na tunaamini viongzi wetu wa ngazi za juu haswa mhe. Rais sisi kama wananchi wa kata ya kia ,tunaamini halifahamu jambo hili ,hivyo tunaomba kama inawezekana tunamuomba aje mwenyewe azungumze na wananchi au atume watu waje wazunguke hili eneo wajue.Alisema diwani.
 
Akizungumza kwa niaba ya wanawake ni Elishia Mollel alisema kuwa mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwaweka katika wakati mgumu
 
Huu mgogogoro kila mwaka unaibuka ,tunamuomba mhe.Rais kuingiliakati maana tumekuwa tunakosa amani kwani sisi wananchitunaozunguka uwanja wa ndege tunapata mateso makubwa usiku hatulali tunakuwa na wasiwasi sana kilamara tunaambiwa tuhame kutoka eneo hilo,jambo ambalo siyo sawa kwani wananchi waliopo katika maeneo hayo ni wa muda mrefu.Anasema Naishie Mollel 
 
Anaendelea kusema maeneo hayo hakuna mgeni bali wapo wenyeji na wamewazika Ndugu na jamaa,anasema tayari uwanja wa ndege tayari waowameshatengewa eneo lao,cha kushangaza ni kwamba wananyimwa kufanya shughuli za kimaendeleo ,sisi hatuchukiii maendeleo la hasha ,bali wanasikitishwa hata zile nyumba ilizowekwa alama ya X wao watakwenda wapi na watoto wao?.Aliuliza swali kwa msisitizo bi Nishie   
 
Kwakweli tumechoka haswa ukizingatia mateso mengi tunapata wanawake na watoto hivi tutakwenda wapi?Mhe.Rais ni mwanamke mwenzetu tunamuomba alitazame jambo hili kwa jicho la tofauti,Tuakuomba chondechonde njoo mama yetu uje uone mwenyewe njoo Kata yetu ya Kia.Alisema Nishie

Akizugumza kwa niaba ya wanawake wenzie amesema kuwa mgogoro huo umekuwa kila mwaka jambo ambalo linawanyima amani wanakuwa na wasiwasi mara zote eneo hilo limekuwa na mgogoro muda mrefu hivyo wanamuomba Mhe.aweze kuwatataulia ili wajue hatma yao.
 

Hata hivyo amesema hapingani na uwekezaji kwakuwa ni suala
lisiloepukika katika kuleta maendeleo ila amewataka wanaokuja kuwekeza
kufuata taratibu,  sheria  na kuwashirikisha wananchi katika hatua za
awali ili kuzuia mgogoro unaoweza kujitokeza.
 
 ” Sisi wananchi tumetakiwa kutofanya ujenzi wa
nyumba za kudumu  katika eneo hilo mpaka watakapopata taarifa kamili ya
maamuzi yatakayotolewa baada ya kupitia nyaraka mbali mbali
zinazoonyesha kuwa KADCO ni wamiliki halali  wa eneo hilo na kupitia
taarifa za wananchi walizotoa kwa kuzingatia  historia na uasilia wa
eneo hilo.alisema
 
 
Kwa upande wake mkuu wa Hai Juma Irando alisema kuwa anaufahamu mgogoro huo,hivyo amewataka wananchi
hao kuwa wavumilivu wakati tatizo lao linashughulikiwa na kuwaahidi
kuwa tatizo hilo linashughulikiwa na wanategemea  litapata suluhu ya kudumu.
 
Amesema kuwa  changamoto hiyo ya kuwekwa alama za ‘X’ kwenye nyumba zao waondoe hofu na wawe na utulivu kwani serikali inashughulikia serikali  suala lao.
 
Akitoa historia ya mgogoro huo mmoja wa wananchi anaeleza kuwa eneo la kia lilitengwa kiserikali mwaka 1970 kwaukubwa wa hekta 11,085 sawa na kilometa  za mraba 110 na mchoro pamoja na uwekaji wa mawe ya mipaka kufanyika 1989 huku hati miliki kwa mamlaka ya viwanja vya ndege ikitolewa 2006  
 
Ramani hiyo ya uwanja wa ndege kwa kiasi kikubwa imechukua sehemu kubwa ya maeneo ya vijiji ambvyo vilivyoandikishwa wakati huo wa operesheni vijiji vya ujamaa kati ya mwaka 1975 na mwaka 1999 kutegemeana na jinsi vilivyoanza kwani vingine vilizaliw kutoka katika vitongoji ndani ya vijiji vya awali.
 
Ramani ya vijiji vyote hivyo ilitolewa mwaka 2006 ambapo nayo ilikuwa na makosa makubwa kwa kuwa  ilipita juu ya ramani ya awali ya uwanja wa ndege bila kuonesha uwanja huo wa ndege.alimalizia kusema mtoa historia fupi.
 
Mwisho