WADAU wa nchi wanachama zinazozungumza lugha ya Kifaransa nchini wamekutana katika kituo cha utamaduni cha ubalozi wa Ufaransa Allience franciese katika kuzungumzia uzinduzi wa kusherehekea wiki ya lugha ya Kifaransa ‘francophonie.
Akizungumza mbele ya wawakilishi wa nchi hizo zinazozungumza lugha ya Kifaransa wakiwamo mabalozi 13 ambao ni wanachama wa jumuiya ya kimataifa ya francophonie (OIF) balozi wa Ufaransa nchini Nadil Hajloui amesema watasherekea lugha ya Kifaransa na francophonie kwa lengo la kukuza lugha hiyo.
Amesema anuai ya lugha na kitamaduni ambapo katika hafla hiyo, wanachama husika wamepanga mfululizo wa matukio ya bila malipo ambayo yataendeshwa kwa zaidi ya wiki mbili kuanzia jumatano machi 9 hadi 26. 2022.
Hajloui alitaja baadhi ya nchi wanachama ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa kuwa ni Ubeligiji,Burundi,Kanada,Congo,Comoro,Misri,Ufaransa ,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Morocco, Rwanda, Senegal, Seychelles, Uswisi,na Vietnam ambao hao wote ni wanachama wa Jumuiya ya kimataifa ya Francophonie.
Akizungumzia matukio hayo amesema kutakuwa na Tamasha la walewale, kundi franco -Tanzania ,litatumbuiza katika jukwaa la Allience Francaise Dar es Salaam siku ya jumatano machi 9 ,mchana. Onesho la filamu ya Tapis Rounge”(red Capet”) iliyopendekezwa na ubalozi wa Usisi ambayo itaononyeshwa kituo hapo jumatano machi 11 jioni.
Pia amesema maonyesho ya sanaa na Tamasha .tamasha la fariji, bendi ya kikongo ,makadirio ya filamu uhuishaj ya Kanada iliyopendekezwa na ubalozi wa Kanada na kuoneshwa Allience Francaisee Dar es Salaam na itafuatiwa na conktail.
Hata hivyo wawakilishi hao wakizungumzia historia fupi na muktadha wamesema waazilishi wa shirika la kimataifa la francophonie ( OIF) walikuwa leoppold S. senghor Rais wa zamani wa senegal .Habib Bourguib na Hamani Diori wenzake wa Tunisia na Nigeria pamoja prince Norodom Sihanouk wa Cambodia.
” lengo lao lilikuwa kutumia lugha ya Kifaransa kama njia ya kukuza mshikamano na maendeleo, na kuleta jumuiya mbalimbali pamoja. Maono yao yalitimia ilipofika machi 20, mwaka 1970 huko Niamey (Niger) ambapo mataifa 21 na serikali zilitia saini mkataba wa kuunda wakala wa ushirikiano wa kitamaduni na kiufundi (ACCT).
Nakwambia Kifaransa kilikuwa kitovu cha shirika kwa lengo la kupanua mawasiliano ya kiutamaduni na kiufundi kwa wanachama na mwaka 1998 ACCT ikawa shirika la kiserikali la francophonie na tangu 2005 imekuwa ikijulikana kama OIF na tarehe ya kuundwa kwa ACCT machi 20 ilichaguliwa mwaka 1998 kuadhimisha siku ya kimataifa ya francophonie OIF.
“OIF ni chombo chenye nguvu cha ushirikiano na kubadilishana kitamaduni kati ya wanachama wake, haswa kwa kukuza lugha ya Kifaransa na anuai ya lugha na kitamaduni, lakini pia kwa kushirikiana katika nyanja zingine kama vile amani, demokrasia na haki za binadamu na msaada kwa kielimu, mafunzo,elimu ya juu na utafiti.
Nakuongeza kuwa Leo OIF inajuisha nchi 54 wanachama, wanachama 7 washirika 27 waangalizi zilizoungana katika hatima moja zinazotoka kukuza na kuendeleza lugha ya Kifaransa kupitia jamii yao bila kujali kama Kifaransa ni lugha yao rasmi au la
Kuhusu lugha ya Kifaransa wadau hao wamesema kuwa ni lugha ya tano (5) inayozungumzwa zaidi duniani. na kwasas kuna wazungumzaji zaidi ya milioni 300 duniani kote na kufikia 2070 idadi ya wazungumzaji wa lugha ya Kifaransa inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 800 ni lugha rahisi katika nchi 32na katika mikoa na idara zote za Ufaransa za nga,ambo inatumiwa katika mashirika mengi ya kimataifa pamoja na umoja wa Afrika.
Mabalozi hao pia wamesema Kifaransa inachukuliwa kuwa lugha ya kimataifa ya kidiplomasi .inasalia kuwa lugha ya pili ya kidiplomasia kwa taasisi nyingi za kimataifa, nilugha ya kufundisha kwa zaidi ya watu milioni 132 na lugha ya nne inayotumiwa kwenye mtandao. na ni lugha ya pili ya kimataifa inayotumiwa zaidi katika vyombo vya habari na muhimu zaidi, lugha ya tatu muhimu ya biashara na watanzania ni zaidi ya watu milioni 1.5 wanazungumza Kifaransa hususan maeneo ya kigoma.
Kuhusu Tanzania wadau hao wamesema idadi inayoongezeka ya wanafunzi na wataalamu wanajifunza Kifaransa .Nia hii ya lugha ya Kifaransa inaweza tu kusifiwa katika nchi ambayo ina majirani kadhaa wanaozungumza Kifaransa na ambayo imeonyesha dhamira yake kubwa ya kushiriki katika ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa wa Afrika.
Tanzania inashiriki mpaka wa nchi kavu na baharini na nchi tatu wanachama wa francophonie Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na rwanda .ikiwani vitajumuisha visiwa vya Mayotte na Reunion, ambavyo ni maeneo ya ng’ambo, ya Ufaransa. Lugha ya Kifaransa pia inahushwa na bahari ya hindi, ama na pwani ya Tanzania bara au visiwa vya zanzibar.
Kwa upande wake balozi wa Congo
Profesa Jean Kitembo amesema lugha ya Kifaransa ni kiunganishi kikubwa cha amani na utulivu duniani na kwa upande wa kwao jamhuri ya congo lugha hiyo inaanza kufundishwa kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.
Amesema Kifaransa ni miongoni wa lugha kubwa ambazo zinazozungumzia nchi Congo ikiwemo la lugha ya kiswahili, kilingara, na lugha nyingine hivyo wiki hiyo ya kusherekea francophonie ni muhimu kwa ustawi harisi wa kutambua umuhimu wa lugha ya Kifaransa.