Watuhumiwa mauaji ya katibu wa kanisa katoliki wapandishwa mahakamani

Njombe

Na Mwandishi Wetu 

Watuhumiwa wa mauaji ya katibu wa baraza la walei kanisa katoliki parokia ya Makambako Nickson Myamba (46) wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe juzi februari 16,2022 kwa Mara ya kwanza.
Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe Matilda Kayombo akitaja shauri namba 5 la mwaka 2022 linalowakabili Daniel Mwilango(42) na Nickson Nyamideko(23).
Hakimu anasema watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika na mauaji ya Nickson Myamba yaliyotokea Februari 7 mwaka huu huko mjini Makambako.
Wakili wa serikali Magdalena Kisoka akisaidiwa na Paul Ngonyani wamesema kosa wanalokabiliwa nalo ni Kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 ya sheria ya makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Aidha hakimu Magdalena Kisoka amepanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo ambapo itakuwa tarehe 28 mwezi Februari mwaka huu kutokana na kutokamilika kwa upelelezi wa shauri hilo.
Hata hivyo watuhumiwa hao wamerejeshwa rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.
Watuhumiwa hao wawili Nickson Nyamwideko na Daniel Mwilango wanashikiliwa kwa tuhuma za kumpiga na chuma na kumkata kwa panga vipande vipande na kusababisha kifo cha Nickson Myamba kilichotokea mtaa wa Mangula Mjini Makambako mkoani Njombe.