Rais samia ang’ara maonyesho ya dubai 2020expo

 HAPPINESS SHAYO NA ABUBAKAR KAFUMBA,UAE

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa miongoni mwa viongozi bora wa kuigwa duniani katika Maonesho ya Dunia yanayoendelea ya Dubai 2020 Expo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akihutubia Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-La Dubai.
Hayo yamesemwa Desemba 14, 2021 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipotembelea banda la wanawake “Women’s Pavilion” katika maonesho hayo yanayoendelea Dubai.
Mhe. Masanja amempongeza Rais Samia kwa kuongoza maendeleo ya nchi ya Tanzania na hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine duniani.
Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Bi. Hafsa Mbanga akichangia mada katika Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi.
Baadhi ya Wanajumuiya ya Wafanyabiashara Dubai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja alipokuwa akihutubia Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akikabidhiwa zawadi na Waziri wa zamani wa Mazingira na Maji UAE, Mhe. Dkt. Mohammed Al Kindi kwa kuthamini mchango wake katika kukuza utalii nchini Tanzania wakati wa Kongamano la Uwekezaji la Sekta ya Utalii lililofanyika hoteli ya Shangri-la Dubai. Anayeshuhudia ni Mwanzilishi & Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Vilabu Duniani, Dkt. Tariq Ahmed Nizami.
Aidha, amewahimiza Watanzania kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Samia katika jitihada za kuleta maendeleo ya nchi ya Tanzania.