Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ngorongoro, Juma Mhina akikabidhi mgombea wa CCM timu ya kuwania nafasi hiyo baada mgombea huyo kupitishwa na chama chake |
Ngorongoro, Novemba 11,2021
Na Mwandishi Wetu
WAGOMBEA wa vyama 13 vya Siasa wamejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Ngorongoro katika uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Disemba 11 mwaka huu.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Willium Ole Nasha kufariki Septemba 27 mwaka huu Jijini Dodoma muda mfupi baada ya kurejea kutoka Jijini Arusha kikazi.
Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro Dk,,Juma Mhina ametaja wagombea hao kuwa ni pamoja na
Emmanuel Shangai (CCM) Simon Bayo (SAU) Singa Kalekwa (CCK), Amina Mcheka (NLD) Mary Daudi (UPDP).
Amewataja wagombea wengine kuwa ni Mgina Mustafa (AAFP),.Frida Nnko (UMD),Paulo Makuru (UDP),Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA),
Simon P Ngilisho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson Gagu (ACT WAZALENDO) na Zuberi Hamis (ADA TADEA).
“Zoezi la utoaji wa fomu lilianza Novemba 9 mwaka huu na mpaka Novemba 11 mwaka huu wagombea 13 kutoka vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini wamejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo ya ubunge”.
Amesema NEC itaendelea kutoa fomu hizo hadi Novemba 15 mwaka huu saa 10:00 jioni na wagombea na siku hiyo hiyo watatafanya uteuzi wa wagombea ambao watakuwa wamekidhi sifa za kugombea ubunge wa jimbo hilo.
“Wagombea wote watatakiwa kurejesha fomu zao Novemba 15 mwaka huu na endpo kuna mgombea yeyote atakayepata changamoto wakati wa kujaza fomu yake ofisi zetu za NEC zitakuwa wazi muda wote kwa ajili ya kutoa msaada kwa wagombea ikiwa ni pamoja na uhakiki iwapo fomu zimejazwa vizuri kabla ya kuzirejesha”.
Amesema baada ya uteuzi utakaofanyika November 15 mwaka huu wagombea watakopitishwa kushiriki uchaguzi huo wataanza kampeni Novemba 16 hadi Disemba 10 mwaka huu na uchaguzi utafanyika Disemba 11 mwaka huu.