Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mratibu wa Tasaf katika Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone amesema tatizo la walengwa wa Tasaf kutolipwa ruzuku yao kutokana na changamoto ya vidole kushindwa kusoma kwenye mfumo wa kielekitroniki imetatuliwa ambapo watalipwa pesa zao kuanzia jumatatu Oktoba 25 Mwaka huu 2021
Amesema hatua hiyo ni maelekezo yaliyotolewa na Tasaf makao makuu ambapo tatizo hilo limetafutiwa njia mbadala hivyo walengwa wote wenye changamoto hiyo watalipwa ruzuku yao kwa pesa tasilimu
Mratibu huyo amesema mfumo wa kielektroniki utaendelea kutumika huku serikali ikiangalia njia sahihi ya kuondoa changamoto hiyo
“Changamoto iliyopo ni watu wenye vidole ambao vinashindwa kusoma kwenye mashine na tukili kwamba sasa ni awamu tatu hawajachukua na tayari Tasaf makao makuu wameshaliona hilo tatizo na wametoa njia mbadala fedha zao watalipwa kuanzia jumatatu na jumanne tunategemea wote tutakuwa tumewalipa huku tukiendelea kulekebisha taarifa kwenye mfumo watalipwa keshi lakini hatuwezi kuepuka kulipa kwa kielekitroniki ndiyo maelekezo ya serikali”amesema Kiwone
Hatua hiyo inafuatia malalamiko ya baadhi ya walengwa wanaonufaika na Tasaf hasa wazee kushindwa kupata ruzuku yao kwa muda mrefu kutokana na mfumo wa kielekitroniki unaotumika hivi sasa kuwa na changamoto ya vidole kushindwa kusoma kwenye mfumo huo