Serikali kusaidia wakulima kufikia ili malengo yao

 Na Rhoda Simba, Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa ipo  tayari kuunga mkono na kutoa kila aina ya msaada unaohitajika ili kuhakikisha  kwamba malengo ya wakulima yanafanikiwa hapa nchini.

Hayo yamesemwa jijini hapa na Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthon Mavunde wakati akifunga maonesho ya wiki ya mavuno yaliyoandaliwa na kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini ( JATU PLC). 

 “Dodoma ni makao Makuu, mahitaji yanaongezeka kwahiyo hata wakulima waongezeke na wajikite katika kilimo biashara, ili kuondokana na ule utamaduni wa kulima mtama na mahindi siku zote ,fursa za kiuchumi zipo  kwenye masuala ya kilimo cha biashara nitafurahi nikiona makundi ya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu wakishiriki” Amesema Mavunde

Wakati huo huo , amesema muamko wa vijana umekuwa mkubwa katika kilimo tofauti na zamani ambapo kupitia mikopo ya halmshauri vijana wamewezeshwa fedha na wanaenda kufanya kilimo hivyo kampuni ya JATU itumie fursa hiyo kutoa elimu kwa vijana namna ya kulima kilimo cha kisasa.  

“Tunashukuru  sana kwa maonesho haya ya JATU kufanyika jijini Dodoma, tunaamini kwamba maonesho haya yataenda kubadilisha  fikra na mtazamo ya wakulima wetu na hasa katika kuwekeza katika kilimo biashara  na namna gani wanaweza wakafanya kilimo cha kisasa na hasa kwa sasa ambapo kilimo mboga mboga kimeonekana kushika kasi” Amesema Mavunde

Kwa upande wake Meneja kutokaTaasisi ya JATU Mohamed Simbano amesema kampuni hiyo ilianzishwa na vijana wa kitanzania ambao ni wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam lengo likiwa ni kuhakikisha ustawi wa maisha ya watu kiafya kutokana na bidhaa bora na asilia zinazotokana na kampuni hiyo.

“Pia inatoa suluhisho katika kupunguza umasikini kwa kutumia ipasavyo  rasilimali watu kilimo cha kisasa na  shughuli za viwanda pamoja na kugawana faida na mlaji wa mwisho”amesema Simbano.

Akizungumzia kuhusu kufunga maonesho hayo Simbano amesema wao kama JATU wanafanya kilimo kiwe sehemu ya kitega uchumi na si kuwa shughuli ya wazee mara baada ya kuustafu na kwa kipindi cha maonesho ya wiki moja wameweza kutembelewa na wakulima na wajasiriamali elfu 9 wakitaka kujifunza namna ya kulima kisasa.

“Kuhitimisha kwa maonesho hayo sisi kama JATU tunaenda kufanya tathimini tunaenda kuhakikisha kwamba  tunaenda kujiridhidha wenyewe Sisi tutaendelea kutengeneza  na tunaendelea kuwasisitiza vijana tuwe wamoja  katika kuleta maendeleo ya nchi yetu” amesema Simbano.

Amesema kama kampuni wameambatana na maafisa ugani  kwahiyo watu waliokuwa wakifika katika maonesho hayo walikuwa wanatatua changamoto  zao kuhusu aina ya kilimo wanacholima.

“Lengo letu ni  maeneo yote  kujifunza namna ya kuimarisha na kuchochea ukuwaji wa sekta ya kilimo kama ilivyo sera ya kilimo na mikakati ya serikali katika kuhimiza taasisi kuweka nguvu katika kilimo kwa kuwa ndo sekta inayochangia katika sehemu kubwa ya pato la taifa”

“Tunaishukuru sana Serikali na uongozi wa jiji la Dodoma kwani mapokeo yamekuwa mazuri tofauti na mikoa mingine tulipowahi kwenda hapa mapokezi na muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa sana wa kuja kujifunza ” amesema Simbano

Hata hivyo maonesho  hayo ya  kilimo kanda ya kati yanamefungwa  tarehe 20 october huku yakiwa yamebebwa na kauli mbiu isemayo” wiki ya mavuno anza na ekari moja”.