Rais samia awasili arusha kwa kishindo, atoa mil10 kusaidia ujenzi zahanati ya kikatiti

Na Seif Mangwangi, Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itatatua changamoto zote za wananchi na kuwataka wasiwe na wasiwasi.

Mhe.Rais Amesema hayo leo Oktoba16,2021 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kikatiti, katika Halmashauri ya Meru, Wilayani  Arumeru alipokuwa njiani kuingia Jijini Arusha akitokea Mkoa wa Kilimanjaro.

Amesema Changamoto zote ikiwemo ujenzi  wa Barabara, Maji na kituo cha Afya cha Kikatiti zote zitafanyiwa kazi.

Ili kuonyesha nia yake njema ya kuhakikisha kata hiyo inakuwa na zahanati,  Mhe. Rais Samia Saluhu ametoa shilingi Milioni 10 zakusaidia kuboresha Zahanati hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akiwa Wilayani Arumeru, Mhe.Rais amesimama na kuwasalimu Wananchi katika maeneo ya Kikatiti, Usa-River na Tengeru.

Akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani Arusha, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili leo kesho Oktoba 17, 2021  atatembelea mradi wa Maji wa Chekereni, atazindua hospitali ya Wilaya Jiji la Arusha na kuzungumza na wananchi katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid.

Aidha Mheshimiwa Rais  atazindua kiwanda cha Nyama Longido, uzinduzi wa mradi wa Maji Longido na atafanya Mkutano wa hadhara stendi mpya Longido.