Uwt shinyanga waadhimisho wiki yao kwa kupanda miti

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya umoja wa wanawake wa  chama cha mapinduzi UWT CCM wilaya ya Shinyanga mjini kimefanyika leo kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

 

Maadhimisho hayo yalianza tangu Septemba 28 Mwaka huu ambapo UWT wilaya ya Shinyanga mjini imeadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo upandaji wa miti 

“Maadhimisho ya wiki ya UWT yanayofanyika kitaifa tumeanza tarehe 28 mwezi wa tisa na kilele chake ni leo 04/10/2021 UWT wilaya ya Shinyanga mjini tumeshiriki kutoa tofali 200 na miti 200 katika kata ya Ibinzamata shule ya msingi Bukweto na ambapo ni ndani ya mwendelezo wa sherehe hiyo na leo tumetoa miti 175 ambayo imetolewa kila kata kwa ujumla wake wilaya ya Shinyanga mjini tumetoa miti 3000 kwa ajili ya kutunza mazingira kwani ni kuendelea kuifanya Shinyanga kuwa ya kijani”amesema katibu Lucy

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Lucy Enock amewataka wanawake wa CCM kuendeleza umoja na mshikamano ili kulijenga Taifa imara huku akiwaomba walimu wa shule ilipopandwa miti kuitunza ili kuhifadhi mazingira

“Wanawake niendelee kuwaasa tuendelee kufanya kazi za umoja wa wanawake tushikamane, tupendene, tuwe wamoja kuhakikisha tunaijenga UWT na hasa katika wilaya ya Shinyanga na Mkoa wa Shinyanga lakini pia natoa rai kwa walimu wote wa shule za msingi na sekondari ambapo tumepanda miti hii waendelee kuitunza ili kuendelea kutunza mazingira ya Shinyanga”

Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo mjumbe wa baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga Rehema Nhemanilo amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya Uviko 19 

“Corona ipo na watu wanakufa tusibweteke mwenyezi Mungu anakusaidia pale unapojisaidia na wewe tuendelee kumuomba mwenyezi Mungu lakini na sisi tuendelee kujikinga mikusanyiko isiyoyalazima tuiepuke lakini pia kunachanjo hata kama tunaambiwa siyo lazima lakini tuhamazishe watu waende wakachanjwe kwahiyo ni maamuzi ya wewe na moyo wako na Mungu wako”amesema Rehema

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ibinzamata Ezekiel John Sabu amewashukuru umoja wa wakinamama kwa kufanya kazi ya kuigwa katika kata yake

“Nimefurahi sana kupata ugeni huu wa UWT wilaya ambapo umekuja kufanya kazi pamoja nasi kwa siku ya leo wamefanya kazi ya kuigwa nawaomba kwa siku nyingine wanapokuja na maadhimisho ya namna hii watuletee kata ya Ibinzamata kwa sababu tunamaandalizi mazuri na tutawapokea kwa kazi hii na Mungu awabariki”