Wanafunzi 100 kuondoa nchini septemba 25 kwenda ukraine, india

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmaliki Mollel akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaotarajia kuondoka nchini hivi karibuni kuelekea Ukraine na India

WANAFUNZI zaidi ya 100 kutoka Tanzania wanatarajia kuondoka nchini Septemba 25 mwaka huu kuelekea India na Ukraine kujiunga na masomo ya vyuo vikuu.

Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL), Abdulmaliki Mollel amesema wanafunzi wanaokwenda kusoma nje wanaangaliwa kwa ukaribu na kampuni hiyo hadi wanapohitimu ili kuweza kumsaidia mzazi kuona thamani ya fedha ya kumsomesha mwanae nje ya nchi.

Mollel aliyasema hayo kwenye mkutano maalum wa kuwaaga wanafunzi 100 wanaotarajia kuondoka nchini kusoma vyuo vikuu vya nchini India na Ukraine ambao wamepitia GEL.

Amesema GEL inafanya kila kitu kwa mwanafunzi anayepitia hapo wanaangaliwa kwa ukaribu tangu hatua ya awali hadi mwisho anapohitimu.

Amesema GEL ni wakala mkubwa wa kupeleka wanafunzi nje ya nchi na imeweza kuwasaidia Watanzania wengi kupata fursa za kusoma nje ya nchi pasipo vikwazo ikiwamo kuwasaidia mikopo isipo na riba.

Mollel amesema wanafunzi hao watasindikizwa kwa ajili ya kuangalia makazi ya wanafunzi pindi wanaposoma katika vyuo mbalimbali.