Wahamiaji haramu wanasema njombe

 NJOMBE

Wahamiaji haramu 12 kutoka Ethiopia waliovikimbia vikosi vya Ulinzi na usalama vya jeshi la polisi na uhamiaji  August 8 katika msako uliofanyika katika eneo la machungio la kijiji cha Uhambule wamekamatwa baada ya kushinda muda mrefu na njaa na kisha kuishiwa nguvu za kuendelea kukimbia katika mapori ya wilaya ya Wanging’ombe

 

Hapo jana vikosi vya Ulinzi na usalama kutoka jeshi la polisi na uhamiaji baada ya kuskia Kuna hali isiyo ya kawaida katika eneo hilo vilifanya msako mkali katika Kijiji kinatajwa kutumika Sana Kama kituo Cha wahamiaji haramu Cha Uhambule kilichopo wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe  na Kisha kufanikiwa kuwashika wahamiaji 26 huku wengine wakifanikiwa kumbilia porini ambapo Leo wamekamatwa Tena.

 

Kamanda kikosi cha uhamiaji kamishna msaidizi mwandamizi John Yindi baada ya kuwakamata watu hao amewapongeza wananchi wa eneo Hilo ambao wamekubali kutoa taarifa ya uwepo wa watu hao aambao walikuwa wakituma watu kuwasaidia kupata chakula mafichoni waliko.

 

“Swala la ulinzi na usalama ni la kila mtanzania kwa hiyo tunaomba muendelee kutoa taarifa kwa viongozi weny wa vijiji mnavyoona watu kama hawa”alisema kamanda Yindi

 

Nae Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa ambaye alilazimika kuingia porini kuwasaka watu hao amesema Jana wamekamata 26 huku 15 wakifanikiwa kuwakimbia ambao Leo 12 wameshikwa ,hivyo wananchi waendelee kupinga uwepo wa watu hao Kijijini kwao kwakuwa hawajui na magaidi au vipi.

 

“Hili eneo watu wameona ni sehemu ya kujificha sasa hivi watu wanaogopa hata kuingia kwenye majani kule,jana wamekamatwa 26 na wengine watano jumla wamekuwa 31 kwa hiyo wako wengi hawa hata ukiwapa basi hawatoshi bado watatu kwa kuwa tumewapata 12,kuna watu wameleta huku na kwa hali kama hii hatuwezi kujua kama ni wema”alisema Kamanda Issa

 

Awali afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Uhambule Yasinta Lupumbwe amesema wamewatia nguvuni watu hao na Kisha kuwaweka katika ofisi ya kata kwakuwa walianza kusimamishwa watu njiani na kuomba wanunuliwe chakula.

 

“Saa nne asubuhi alinipa taarifa katibu wa uhambule kwamba porini kule kuna wahamiaji amekutana nao wakawa wanamuomba awanunulie chakula,tukaongea nao tukajua ni wale wale miongoni ambao walichukuliwa tarehe nane.Wananchi hawa wa kijiji cha uhambule wakaandaa uji na chakula wamekula”alisema Yasinta Lupumbwe