Dkt.fenella mkangara afungua ‘viwango sports bonanza’, ahimiza wafanyakazi wa tbs kushiriki katika michezo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Dkt. Fenella Mukangara akipiga penati akiashiria ufunguzi rasmi wa Bonanza lililokwenda kwa jina la ‘Viwango Sports Bonanza’. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Dkt. Fenella Mukangara akizungumza katika Bonanza la michezo (Viwango Sports Bonanza) lililoandaliwa na TBS ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini. Bonanza hilo limefanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athumani Ngenya akizungumza na kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Dkt. Fenella Mukangara kufungua Bonanza ‘Viwango Sports Bonanza’ lililofanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athumani Ngenya akizungumza na waandishi wa habari katika Bonanza la michezo (Viwango Sports Bonanza) lililoandaliwa na TBS ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini. Bonanza hilo limefanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Wafanyakazi wa TBS wakishindana kuvuta kamba katika Bonanza la michezo (Viwango Sports Bonanza) lililoandaliwa na TBS ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini. Bonanza hilo limefanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo
Moja ya timu ya mpira wa miguu Wafanyakazi wa TBS wakipata picha ya pamoja katika Bonanza la michezo (Viwango Sports Bonanza) lililoandaliwa na TBS ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini. Bonanza hilo limefanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.
Wafanyakazi wa TBS wakishiriki mchezo wa pete katika Bonanza la michezo (Viwango Sports Bonanza) lililoandaliwa na TBS ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini. Bonanza hilo limefanyika katika viwanja wa michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Athumani Ngenya ( katikati) akishuhudia mchezo wa bao kati ya wafanyakazi kutoka Kurugenzi ya Viwango na Kurugenzi ya Udhibiti Ubora katika bonanza la michezo lililofanyika leo viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Shirika la Viwango Tanzania limewakutanisha watumishi wa shirika hilo kutoka maeneo mbalimbali kushiriki Bonanza ambalo litawasaidia kuongeza wigo wa kufahamiana na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza wakati akifungua Bonanza hilo lililoitwa Viwango Sports Bonanza, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Dkt. Fenella Mukangara amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha michezo inakuwa endelevu katika taasisi hiyo ili kuwaweka karibu watumishi wa shirika hilo na kuunda ushirikiano chanya.
“Nitakikisha katika miaka ambayo nitaendelea kuwa mwenyekiti michezo hii inachezwa na ikiwezekana tunaongeza namba ya michezo zaidi”. Amesema Dkt.Mukangara.
Amesema kupitia michezo mbalimbali hasa kwenye mabonanza kutasaidia kujenga na kuongeza mahusiano chanya ya wafanyakazi, kupunguza msongo wa mawazo, kuburudika, pamoja na kuboresha afya za wafanyakazi kwa ujumla.
Aidha Dkt.Mukangara amewahimiza watumishi wa TBS kujitokeza katika vituo vinavyotoa huduma ya chanjo kuweza kupata chanjo ili kujikinga na Ugonjwa wa UVIKO 19 ambao umekuwa tishio ulimwenguni kote.
“Nahimiza kabisa tuchanje, nafasi tumepata ili tuwe wafanyakazi wenye afya bora lakini wenye uhakika wa maisha ili tusije tukakutana katika hali mbaya ya majonzi”. Amesema Dkt.Mukangara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema kuwa lengo la ‘Viwango Sports Bonanza’ kujenga afya ili kujikinga na magonjwa nyemelezi kama vile ugonjwa wa Korona.Pia kwa wafanyakazi ni sehemu ya kupumzisha mwili ili kuongeza kasi ya ufanyajikazi pindi warudipo kazini.