Ng’ombe 6270 wametambuliwa kwa njia ya Kuvishwa Hereni za kielektroniki katika kijiji cha Kitosi Wilayani,Nkasi Mkoa wa Rukwa.
Haya
yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwenye,
Mkutano na wafugaji katika Kijiji cha Kitosi mara baada ya kushiriki
katika zoezi la uwekeji herenikatika kijiji hicho.
Waziri
Mashimba amesema kuwa zoezi la utambuaji wa Mifugo linatekelezwa nchini
kote na kwa sasa tumeanza na mikoa ya Mfano ambayo ni Rukwa ,Katavi ,
na Kigoma.
Amesema
zoezi hili limeanza Katika kijiji cha Kitosi Wilaya ya Nkasi na tangu
zoezi hili limeanza zaidi ya ng’ombe 6270 tayari wameisha tambuliwa kwa
kuvishwa hereni katika kiji hicho.
Amesema
zoezi hili nimuhimu kwa kuwa linaongeza thamani ya Mifugo ya wafugaji
katika Masoko na kusaidia kufuatilia ubora wa mazao yanayo zalishwa na
Mifugo iliyotambuliwa kwa njia ya hereni.
Amefafanua kuwa Mifugo itakayozalishwa itakidhi mahitaji ya soko la nje la Mifugo yetu na mazao yake.