Chuo cha ufundi arusha kipo mbioni kutengeneza gari la umeme

 

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha
(ATC) ,Dkt Yusuph Mhando,akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa chuo
hicho kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya
kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia katika chuo hicho.

Baadhi ya waandishi na wafanyakazi na
wanafunzi wakifatilia wasilisho la Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha
(ATC) ,Dkt Yusuph Mhando (hayupo pichaniu) wakati akiwasilisha taarifa
ya utekelezaji wa chuo hicho kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni
hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha
(ATC) ,Dkt Yusuph Mhando,akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa
Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho
yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho
mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa chuo hicho.

Muonekano wa jengo lililopo katika
Chuo cha Ufundi Arusha mara baada ya maboresho yaliyofanywa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia

Muonekano wa Tenki la Maji lililopo
katika Chuo cha Ufundi Arusha mara baada ya maboresho yaliyofanywa na
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia

Mkufunzi kutoka Idara ya Magari
katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi David Raymond akiwaeleza
Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia
maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika
chuo hicho jinsi walivyojipanga kuanza kutengeneza gari litakalotumia
umeme mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa na Serikali kupitia
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Baadhi ya magari yaliyofanyiwa maboresha katika Chuo cha Ufundi Arusha.

Wanafunzi wakitengeneza mashine ya
kutoa sanitaizer ili kujikinga na ugonjwa wa Corona ambayo mtu ataitumia
bila kugusa maji ama sabuni mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa na
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Muonekano wa mashine zilizopo katika chuo cha Ufundi Arusha

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika
chuo cha Ufundi Arusha ,anaesomea Electrical Biometrical Engineering,
Wema Laurence akielezea maboresho yaliyofanywa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo
yao kwani watafika chuo kwa wakati kutokana na kukaa hosteli ambazo
zipo karibu na Chuo.

Mkufunzi kutoka Idara ya Magari
katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi David Raymond akiendesha
baiskeli iliyotengenezwa katika Chuo hicho mara baada ya kupatiwa vifaa
vya kisasa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu Chuo cha
Ufundi Arusha Leocadia Shirima akiipongeza Serikali kupitia Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kukidhi mahitaji yao kwa upande wa
wasichana baada ya maboresho yaliyofanywa katika Chuo cha Ufundi Arusha

Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha
Mhandisi Abdi Mjema akiwaonyesha waandishi wa habari muundo wa
kutengeneza ndege mara baada ya kupatiwa vifaa vya kisasi na Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika maboresho
yaliyofanywa katika Chuo hicho.

……………………………………………………………………

Na Alex Sonna,Arusha

KUTOKANA na kupatiwa vifaa vya kisasa
na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Chuo cha
Ufundi Arusha (ATC) kipo mbioni kutengeneza gari litakalotumia umeme.

Hayo yameelezwa leo Agosti 12,2021 na
Mkufunzi kutoka Idara ya Magari katika Chuo cha Ufundi Arusha,Mhandisi
David Raymond wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika Chuoni
hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.

Mhandisi huyo amesema maboresho
yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yamewagusa kwa
kiasi kikubwa kwani wameweza kupata vifaa vya kisasa na wanafunzi
wanasoma kwa urahisi na wengi wamekuwa wakielewa kutokana na kusoma kwa
vitendo.

Amesema kwa sasa wameweza kutengeneza
baiskeli pamoja na Helcopta na wapo mbioni kutengeza gari ambalo
litatumia umeme kutokana na kupatiwa vifaa vya kisasa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia..

“Tumetengeza baiskeli yenye kutumia
umeme wa jua na tuna tunaendelea na utengenezaji wa Helcolta ambao upo
katika hatua za mwisho kwa hivi ni vitu ambavyo tumetengeneza kwa sasa
lakini tupo mbioni kutengeneza gari kabisa litatumia umeme, vyote
vinatengenezwa hapa katika idara yetu”amesema Mhandisi Raymond.

Aidha,Mhandishi huyo amesema chuo
hicho kinafundisha ufundi wa umeme wa magari na magari yenyewe ambapo
amedai kuna madhara makubwa kupeleka magari kwa mafundi wa mtaani kwani
wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa kubahatisha.

MABORESHO YA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya
Chuo hicho,Kaimu Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt Yusuphu Mhando amesema chuo
hicho kilianzishwa mwaka 1978 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya ufundi
sanifu katika ngazi ya Cheti(Full Technician Certificate – FTC) ili
kupata wataalamu wenye sifa na ujuzi katika fani mbalimbali za Ufundi.

Dkt Mhando anasema Chuo cha Ufundi
Arusha kilipandishwa hadhi ya kiuendeshaji kupitia Gazeti la Serikali
No. 78 la mwaka 2007 na kufanyiwa marekebisho kupitia Gazeti la Serikali
Na. 302 la mwaka 2015.

Amesema ATC inatoa mafunzo ya ufundi
stadi katika ngazi mbalimbali (level I, II na III) na elimu ya ufundi
kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada katika fani mbalimbali
katika michepuo ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Kaimu Mkuu huyo amasema chuo hicho
kinachoongoza kwa kutoa Mafunzo, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu
vinavyoaendana na mahitaji ya soko kwa kutumia Sayansi, Teknolojia na
Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.

Amesema programu zinazoendeshwa chuoni
hapo zimeanzishwa kwa kuzingatia, Sera za Taifa,Soko la ajira,Azimio la
Kilimo Kwanza,upungufu wa mafundi wa Maabara za Sayansi katika Shule za
Sekondari,Uharibifu wa vifaa tiba hospitalini,Mabadiliko ya teknolojia
na utandawazi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kaimu Mkuu huyo amesema chuo kinatoa Programu za kitaaluma 21 zinazotambuliwa na NACTE na kupewa ithibati.

ZAIDI YA BILIONI 1.4 KWA BWENI LA WASICHANA

Kaimu Mkuu huyo wa amesema Chuo
kilipokea jumla ya shilingi 1.499 bilioni – 14/05/2021 kama ruzuku
kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo
wa kuchukua wanafunzi 420.

“Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Mei,
2021 ambapo utekelezaji umefikia 15% na upo katika hatua za ujenzi wa
msingi (substructure),”amesema.

UJENZI WA MEDICAL CLINIC

Kaimu huyo Mkuu wa Chuo amesema ili
kuwapatia wanafunzi na watumishi huduma za afya na kwa haraka chuo
kilianza ujenzi wa kliniki kwa kutumia mapato yake ya ndani

Amesema Mradi ulianza mwishoni mwa
mwezi Aprili, 2021 ambapo utekelezaji umefikia 30% na upo katika hatua
za ujenzi wa msingi mkubwa (superstructure-framed structure)

UJENZI WA JENGO LA MADARASA NA MAABARA

Amesema Ujenzi ulianza Machi 2018 na
mpaka Disemba 31, 2019 utekelezaji ulifiia 49%. Mkandarasi aliondoka
site na Wizara inashughulikia upatikanaji wa fedha za kumalizia jengo
kwa force account.

BILIONI 37 MRADI WA NISHATI JADIDIFU

Amesema mradi wa East Africa for
Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP)’ inalenga
uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Nishati Jadidifu.

Amesema thamani ya mradi ni Shilingi
37.4 billion , ambapo Chuo kimeshapokea shilingi 11.2 billion ambayo ni
30% ya fedha yote ya mradi kama kianzio.

BILIONI 7 MRADI WA INNOVATION ENERGY EDUCATION PROGRAM (IEEP)

Amesema IEEP ni mradi unaofadhiliwa na
Wizara ya elimu ya Korea ambapo Mradi huo una thamani ya Shilingi
bilioni tano kwa kipindi cha miaka saba kuanzia Aprili 2020 mpaka Machi
2027.

Amesema ATC inashirikiana na vyuo viwili vya Korea -Hanyang University na Seoul National University katika kutekeleza mradi huo.

MABORESHO YAWASAIDIA

Kwa upande wake mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza katika chuo hicho,anaesomea Electrical Biometrical Engineering,
Wema Laurence amesema maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi
na Teknolojia yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao kwani
watafika chuo kwa wakati kutokana na kukaa hosteli ambazo zipo karibu na
Chuo.

“Tunaishukuru Serikali wameanza
kutujengea hosteli mpya ambazo zitatuwewezasha sisi kufika darasani kwa
wakati, ambao tulikuwa tunakaa nje tunapata changamoto za usafiri
tunachelewa kufika sasa hivi tutakuwa tunafika kwa wakati,”amesema.

Kuhusiana na kusoma masomo ya
umeme,anasema ndoto zake zilikuwa kuja kuwa Inginia hivyo alivyofika
chuoni hapo na msukumo wake ulikuwa katika masomo ya Sayansi alimua
kujiunga na kozi ya umeme.

“Mimi nilikuwa napenda umeme na
nilivyokuja hapa chuo nikakutana na Biometical nikaelezewa jinsi ilivyo
na walionitangulia nikaipenda nikaamua kuingia kwenye
Biometical,”amesema

WATENGENEZA MASHINE YA KUTOA SANITAIZER

Amesema wametengeneza mashine ya kutoa
sanitaizer ili kujikinga na ugonjwa wa Corona ambayo mtu ataitumia bila
kugusa maji ama sabuni.

“Na hii inasaidia kupunguza maambukizi
ya Corona kwa sababu Corona inaambukiza kwa kushikana au kwa
kusogeleana,Chuo chetu kina wanafunzi na walimu wengi hivyo inatusaidia.
Hii mashine imefikia hatua nzuri tunachomalizia ni kufunga ‘sense’
mashine zetu tumezitengeneza kidigital zitakuwa zikitumia solar hivyo
zitakuwa zikijichaji huku zikiendelea kutumika,”amesema.