Tanga uwasa yakutana na wadau kupata maoni ya mkataba wa huduma kwa mteja

 

 


MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika leo kwenye ofisi zao za Mwakidila Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed kushoto Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga Saumu Bendera


Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga Saumu Bendera akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni MKURUGENZI wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akifuatiwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa Alawi Ahmed


Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein Ubbena akizungumza wakati wa mkutano huo


Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akizungumza wakati wa kikao hicho

Sehemu ya watendaji na madiwani wa Viti Maalumu (CCM) wakifuatilia kikao hicho

MKUTANO
wa Wadau wa Tanga Uwasa kwa ajili ya kupata maoni kuhusu mkataba wa
huduma kwa mteja ambao umefanyiwa marejeo mwaka 2021 umefanyika leo
Jijini Tanga kwa kuwashirikisha Madiwani wa viti Maalumu,Maafisa Tarafa
wa Jiji la Tanga na Maafisa Watendaji wa Kata.

Akizungumza
wakati akifungua mkutano huo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema
wameamua kukutana na viongozi hao kwa sababu wana watu wengi ambao
wanawawakilisha na maoni yao ni kwa ajili ya wananchi wote na sio yao
tu.

Alisema kwa sababu wao ndio viongozi waliopo kwenye maeneo
hayo hivyo wajitahidi kuhakikisha ushiriki wao kwenye mkutano huo
unakuwa na tija kubwa na sio bora mambo yaende hivyo hakikisheni
mnatumia vizuri uwepo wenu.

“Tunazungumzia mkataba wa huduma kwa
mteja amesema mwenyekiti hapa ni utawala bora lazima mnapokuwa mnapeana
huduma muwe na kitu ambacho kinawaunganisha na kitu kinatuunganisha ni
huu mkataba haki na wajibu wa pande zote mbili mtoa huduma na mpokeaji
wa huduma “Alisema

Alisema wawasilishaji wa mada watawapitisha
ili iwe rahisi kwenu kueleza muundo wa mkataba upoje?haki na wajibu
upoje,zawadi na adhabu zipoje na mwisho wa siku ukikiuka mkataba
tunakufanyaje hayo mambo yote inabidi tuyajadili kwa pamoja leo
hapa“Alisema

Aidha alisema huo mkataba ni kwa wale watu ambao
wana huduma na wale ambao bado hawana maana mwisho wa siku wataomba kwa
ajili ya kuunganishiwa maji kwa sababu kuna vitu ambavyo anapaswa
kufanya yeye na mtoa huduma na ukishafahamu hivyo itakuwa rahisi.

“Hiki
ni kikao cha wadau tunakaa kwa ajili ya kupitia kwa sababu ni zoezi
shirikishi na watakapomaliza hapo wataenda kukutana na wadau wengine
halafu baada ya maoni yao yakishafanyiwa kazi yatapelekwa kwa mdhibiti
Ewura kwa ajili ya kupitishwa rasmi na baadae watatengeneza vitabu
watavigawa kwa wadau wao kwenye ofisi mbalimbali ikiwemo za Kata na
watatoa nakala za kutosha ili kila mmoja aweze kupata.

Awali
akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni
Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Chumbageni (CCM) Jijini Tanga Saumu
Bendera alisema madhubuti ya mkutano huo ni kupitia maboresho ya mkataba
kwa wateja .

Alisema kama wanavyojua maboresho mkataba ni
kwamba mteja kuna haki na wajibu na pia vilevile mtoa huduma hivyo ni
jambo jema ambalo linawapa wigo mpaka wa kutambua mambo mbalimbali.

Alisema
kama wanavyojua Serikali imekuwa ikifanya maboresho ya kila siku na huo
maana yake ni utawala bora kwa hiyo wamefika kama wadau kuweza
kusikiliza maboresho hayo na wao wajue haki zao na wajibu wao na pia
mtoa huduma na baadae watapitia na kuchangia.

Naye kwa upande
wake,Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akizungumza katika
mkutano huo wakati akiwasilisha mada ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa
Tanga Uwasa.

Alisema kwamba mkataba wa huduma kwa mteja
unatakiwa kufanyiwa maboresho kila baada ya miaka mitatu na maboresho
hayo yanapofanyika lazima wadau wahusishwe kuhusiana na nini ambacho
kinajiri.

Alisema watawapitisha kwenye mkataba wote ili wapate
kufahamu na kuona huo mkataba umehusisha nini na nini na maeneo gani
ambayo yamefanyiwa maboresho.

Awali akizungumza wakati
akiwasilisha mada kuhusu Haki na Wajibu wa Mteja Tanga Uwasa Mkuu wa
Kitengo cha Uhasibu Tanga Uwasa CPA Hussein Ubbena alisema lengo la
mkutano huo ni matakwa ya sheria kwamba serikali inataka Taasisi zake
zote zinazotoa huduma ziwe zinaingia mikataba ya huduma bora na wateja
wake hivyo leo walikuwa wanatimiza takwa hilo la kisheria.

Alisema
kwamba Mamlaka iliandaa mkataba wao wa kutoa huduma na leo wamefanya
wasilisho kwa wadau ambao ni watendaji wa serikali za mitaa na madiwani
viti waliwasilisha mkataba ambao waliitengeza kama drafti ili waweze
kupata maoni yao jinsi ya kuuboresha na hatimaye uweze kutumika.

Mwisho.