Mkuu
wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa
madawati,viti na meza kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti Longuza
Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na Ofisi za
Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na Wakala wa
Misitu Tanzania ( TFS)
Mkuu
wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa
madawati,viti na meza kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti Longuza
Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na Ofisi za
Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na Wakala wa
Misitu Tanzania ( TFS)
MKUU
wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo kulia akimkabidhi msaada huo Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza mara baada ya kuvipokea kulia ni
Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
MKUU
wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo ya
makabidhiano iliyofanyika wilayani humo kulia ni Mhifadhi wa shamba la
miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhianoMKUU
wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na Mhifadhi wa shamba
la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kulia akifuatiwa na Meneja
Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo
Sehemu ya madawati yaliyotolewa
NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA
WAKALA
wa Huduma za Misitu TFS shamba la Lunguza lililopo wilayani Muheza
mkoani Tanga wametoa msaada wa madawati, viti na Meza vyenye thamani ya
sh mil17. 4
Msaada huo ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na
Sekondari Tatu ambazo ni pamoja na Ofisi za watendaji kata mbili
zilizopo wilayani Muheza utasaidia kuondosha changamoto zilizokuwepo
awali.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima
Bulembo, Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
alisema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa
huduma.
“Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari” alisema Mwasalanga.
Awali
akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo aliishuku TFS kwa
namna walivyothamini elimu ya Watoto wa kitanzania na hivyo kwa msaada
huo wataweza kuboresha utoaji wa elimu.
Mkuu huyo wa wilaya
alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuilinda
misitu kuhakikisha hakuna uharibu unaofanyika.
“Niwaombe
wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha
tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi”
alisema DC Bulembo
Naye kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa
Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama alisema wametoa madawati
60 ambapo kati ya hiyo madawati 30 wametoa kwenye shule ya Msingi
Kwemdimu, madawati 30 shule ya Sekondari Potwe na madawati 30 wametoa
shule ya Sekondari Amani.
Alisema pia wametoa viti na meza 17
ambavyo wametoa ambapo thamani hizo ni sh.milioni 17.1 wao kama
wahifadhi wanasema wahifadhi wa baadae ni watoto wadogo ambao
wamewatolea thamani hizo.
“Misaada hiyo wanayoitoa kwa shule
hizo na ofisi za watendaji tunaomba thamani hizo zitunzwe pamoja na
walimu waangalia watoto namna wanavyocheza kwa sababu wakati mwengine
wanaweza wakawa wanabonda madawati ili nao kama wakala wa huduma za
misitu Tanzania (TFS) waweze kupata nguvu ya kuendelea kutunzwa
zaidi”Alisema