Tbs yaadhimisha siku ya ithibati duniani

 

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Lazaro Mwambole
akifungua maadhimisho ya siku ya Ithibati duniani yaliyofanyika makao
makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam mapema leo.


Afisa udhibiti ubora mwandamizi Bi.Stella Mrosso akiongea na wadau wa
masuala ya ithibati wakati wa maadhimisho ya siku ya ithibati duniani
mapema leo makao makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam na kauli mbiu
ya mwaka huu ni “ithibati kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo
endelevu ” Wadau
wa masuala ya ithibati wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya
ithibati Duniani mapema leo Makao Makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es
salaam na kauli mbiu ya mwaka huu ni “ithibati kwa utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu “.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)




NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Katika
nchi zilizoendelea kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa malengo ya ajenda
2030 ya maendeleo endelevu hufanikiwa kwa kutumia viwango pamoja na
huduma zinazotolewa na taasisi zenye ithibati ya Umahiri kwenye
upimaji,Ugezi, Ukaguzi na uthibitishaji Ubora.


Katika
nchi hizo ithibati ya Umahiri hutumika kama kigezo muhimu kuondoa
vikwazo vya kibiashara na kukuza uchumi wa nchi, kukuza pato la taifa na
kupunguza umasikini.


Ameyasema
hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
Bw.Lazaro Mwambole katika maadhimisho ya Siku ya Ithibati
(Accreditation) Duniani katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es
Salaam..


Aidha Bw.Mwambole amesema Mamlaka zinazotoa ithibati ya umahiri hufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa wala kuwa na upendeleo.


“Mamlaka
hizi zinatekeleza wajibu wao bila kupendelea taasisi zinazozikagua kwa
ajili ya kupata cheti cha ithibati au wateja wanaohudumiwa na taasisi
hizi”. Amesema Bw.Mwambole.


Amesema
kuwa ithibati ni moja ya nguzo tatu za miundombinu ya ubora, nyingine
zikiwa ni viwango (Standard), Vipimo (Metrology) na udhibiti ubora
(Conformity assessment) ambao hujumuisha ukaguzi, upimaji na
uthibitishaji ubora.