Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina
Ishengoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata
ya Chipogolo wilayani Mpwapwa wakati kamati hiyo ilipotembelea kijijini
hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi na wananchi kuhusu maendeleo
ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akijibu
maswali ya wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata ya Chipogolo
wilayani Mpwapwa wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na
Maji ilipotembelea kijijini hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi
pamoja na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara hiyo
imefanyika leo Juni 19,2021.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Msisiri wakifatilia hotuba mbalimbali wakati
wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,ilipofanya ziara ya
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata ya
Chipogolo wilayani Mpwapwa pamoja na kusikiliza kero za wavuvi na
wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni
19,2021.
Mfanyabiashara
wa Kijiji cha Msisiri Bi.Nelly Athuman akitoa maoni yake kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijiji hicho
kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Juni 19,2021.
Mtendaji
wa Kijiji cha Msisiri Bw.Allan Kayanda,akielezea changamoto zilizopo
katika kijiji hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na
Maji ilipotembelea kijiji hicho kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma
leo Juni 19,2021.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde (CCM) akitoa mapendekezo yake kwa
wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma
mara baada hiyo kutembelea kijiji hicho kuhusu Maendeleo ya Bwawa la
Mtera leo Juni 19,2021.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala,akitoa maoni yake kwa
kamati hiyo amabyo ilifanya ziara ya kutembelea kijiji hicho kuhusu
Maendeleo ya Bwawa la Mtera leo Juni 19,2021.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani
Dodoma wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
ilipotembelea kijijini hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi pamoja
na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara hiyo imefanyika leo
Juni 19,2021.
Muonekano wa Bwawa la Mtera.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina
Ishengoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi
wilayani Iringa Mkoani Iringa baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya
kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi hao kuhusu maendeleo ya Bwawa
la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid
Tamatamah,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi
wilayani Iringa Mkoani Iringa baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya
Kilimo,Mifugo na Maji kufanya ziara ya kuzungumza na kusikiliza kero za
wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni
19,2021.
Mvuvi
wa Samaki Bw.Amir Kiselo,akitoa maoni yake kwa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini cha Mnadani Kata
ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la
Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Afisa
Uvuvi Kata ya Izazi Onesmo Peter,akielezea changamoto wanazozipata
wavuvi katika Bwawa la Mtera kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,
Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani
Iringa Mkoani Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara
iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Mama
Ntilie Bi.Mary Mgata ,akitoa shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Kilimo, Mifugo na Maji mara baada ya kuwatembelea na kuwasikiliza kero
zao wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani
Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni
19,2021
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa
Mkoani Iringa wakiisikiliza Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na
Maji,ilipofanya ziara ya akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu
maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Na.Alex Sonna,Iringa
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na elimu
iliyotolewa kuhusu uvuvi haramu kwa wavuvi wa Bwawa la Mtera.
Hayo
yamesemwa leo Juni 19,2021 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt.
Christine Ishengoma baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika kijiji
cha Msisiri wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kijiji cha Mnadani wilaya
ya Iringa ambapo wamezungumza na wavuvi na wananchi wa maeneo hayo.
Dkt.
Ishengoma amesema katika vijiji vyote walivyopita wamekuta wavuvi na
wananchi kwa ujumla wanayo elimu kuhusu uvuvi haramu na wanashiriki
katika kudhibiti kwa kukamata nyavu haramu na kuziteketeza.
”Kwa
kweli sisi kamati baada ya kuzungumza na wananchi pamoja na wavuvi wa
maeneo yote hayo mawili tuliyotembelea tumeridhishwa na elimu
iliyotolewa kuhusu uvuvi haramu kwa wavuvi wa Bwawa la Mtera”amesema
Dkt.Ishengoma
Hata
hivyo Dkt.Ishengoma amewataka wavuvi kuendelea kudhibiti uvuvi haramu
katika Bwawa hilo ambalo kwa sasa samaki wamepungua katika baadhi ya
maeneo kutokana na Uvuvi haramu.
Dkt.
Ishengoma amewaahidi wananchi wa kijiji cha Mnadani kuwa atalifikisha
tatizo la wingi wa viboko katika Bwawa hilo kwa Waziri wa Maliasili na
Utalii ili aweze kulishighulikia.
Kwa
upande wake Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya
Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa wizara imekuwa ikitoa elimu
kuhusu uvuvi haramu na madhara yake kwa wavuvi na wananchi
wanaolizunguka Bwawa la Mtera ambapo kwa sasa wananchi hao wamekuwa
wakishirikiana na serikali kudhibiti na kuteketeza nyavu zisizofaa
zilizokamtwa.
Dkt.
Tamatamah amewaahidi wavuvi wa kijiji cha Msisiri kuwaletea injini moja
ya boti mwezi Julai, 2021 ambayo pamoja na shughuli za uvuvi
itawasaidia katika kufanya doria za kudhibiti uvuvi haramu.
Pia
amesema kuwa atawatuma wataalam wa utafiti kutoka TAFIRI kuja kuangalia
kutafiti Kama upo uwezekano wa kuweka mbegu ya samaki ili kusaidia
kuongeza wingi wa samaki katika Bwawa hilo.
Dkt.
Tamatamah amewasisitiza wavuvi kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili
waweze kukopesheka na kuweza kupata zana sahihi za uvuvi ambazo mara
nyingi hutolewa na wizara.
Naye
Mkazi wa kijiji cha Mnadani kata ya Izazi wilayani Iringa, Bw. Amiri
Kiselo ameieleza kamati hiyo kuwa viboko katika bwawa hilo wameongezeka
na wamekuwa wakijeruhi na hata kuwauwa wavuvi na kuwafanya kushindwa
kwenda kuvua Samaki.
”Tatizo
hili limefanya samaki kuwa wachache katika masoko na kuwafanya wavuvi
kutafuta shughuli nyingine za kuwaingizia kipato na hivyo ameiomba
kamati kuwasaidia kulitatua tatizo hilo.
Wananchi
katika vijiji vyote viwili wameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge na
wizara kwa kuwatembele na kusikiliza matatizo waliyonayo na wanaomani
kuwa matatizo yao yatatafutiwa ufumbuzi.