Kampeni ya tigo green for kili yapamba moto, wadau wazidi kuchangia miti

 Na Mwandishi Wetu

 Jumatano Juni 3, 2021, KAMPUNI inayorahisisha maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imepokea miche 7,000 ya miti kutoka Helios Towers Tanzania, ikiwa ni mchango wa upandaji miti wa kampeni ya Tigo Green For Kili.


 Kampeni hiyo ni kwa ajili ya kupanda miti kwenye eneo la Mlima Kilimanjaro ya Tigo Green For Kili ambayo mikakati yake ni kupanda miti 28,000, maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro.


 


Kampeni hiyo ilizinduliwa Februari mwaka huu ambapo Tigo imeshapokea michez kutoka kwa wadau mbalimbali.


 


Miche 7,000 ya miti imetolewa na Helios Towers Tanzania, ambapo tayari kampeni hiyo imeshakusanya mchango wa miche 31,446 kutoka Tigo na wadau mbalimbali kwa ajili ya kampeni ya Tigo Green For Kili.

Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya waandishi wa habari katika Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya alisema: “Ni imani yetu kuwa miti hii itasaidia kurejesha sehemu ya theluji kwenye Mlima Kilimanjaro ambayo tumeshuhudia ikipungua kwa miaka minne iliyopita kwa sababu ya ongezeko la joto duniani.


“Ninawashukuru Helios Towers Tanzania kwa kuchangia miche ya miti  7,000 katika kampeni hii. Ninawaomba wadau wengine wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuhakikisha tunafikia malengo kwani tunaendelea kupokea miche.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Helios Towers Tanzania, Ramsey Koola alisema, Helios Towers ina jukumu muhimu katika kuwezesha na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali.

Alisema mikakati yao ni kuhakikisha kukuza na kuendeleza miundombinu ili kupunguza mzigo wa mazingira kwa jamii.

Alisema mkakati huo ni endelevu kwa ajili ya kuchangia masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na mazingira, ikiwemo kuthamini wadau wao.