Serikali kuendelea kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wadogo nchini

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu
wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma
alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila
Mkumbo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akisisitiza jambo kwa washiri wa
Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini
Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara
Prof.Kitila Mkumbo

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO)
uliofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akifurahia jambo na Mlezi wa umoja wa
Mafundi Cherehani Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
Mhe.Anthony Mavunde (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO)
uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na
Biashara Prof.Kitila Mkumbo

Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba
ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil T.
Abdallah,(hayupo pichani) wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa
Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa
akimuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Dkt. Hashil T. Abdallah,akifatilia mada zilizokuwa
zikiwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma
(UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma alipokuwaa akimuwakilisha Waziri wa
Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo.

Mlezi wa umoja wa Mafundi Cherehani
Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde
akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma
(UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma

Mwenyekiti wa umoja wa Mafundi
Cherehani Dodoma (UMACHEDO) Bw.Sadoki Kasuka,akielezea umuhimu wa umoja
huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO)
uliofanyika jijini Dodoma

Mlezi wa umoja wa Mafundi Cherehani
Dodoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde
akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa
Mkutano Mkuu wa Mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini
Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na
Biashara Dkt. Hashil Abdallah,amesema kuwa Serikali itaendelea
kuwezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kupata mafunzo ya
kuendesha shughuli zao pamoja na kuwapatia mitaji ili kutimiza azma ya
serikali ya viwanda.

Dkt.Abdallah
ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mafundi
Cherehani Dodoma (UMACHEDO) uliofanyika jijini Dodoma.

Dk. Abdallah amesema
kuwa serikali ipo tayari kuwezesha wajasiriamali kufanya shughuli zao
bila ya kuwepo na kikwazo chochote kwa mujibu wa sheria ili waweze
kufikia malengo yao.

“Wajasiriamali
wamekuwa wakilalamika kuwa moja kati ya changamoto wanazokabiliana nazo
ni pamoja na elimu ya biashara pamoja na mitaji, hili sisi kama serikali
tutahakikisha tunalifanyia kazi kupitia taasisi yetu ya Sido kwa
kuendesha mafunzo na kutoa mitaji kwa kuzingitia vigezo”amesema Dk.
Abdallah

Pia amesema kuwa
pamoja na kutoa mitaji na elimu pia kupitia Sido wataendelea kuwezesha
wajasiriamali nyenzo zenye ubora ili kuzalisha bidhaa zenye ubora.

“Mfuko wetu wa
kuwezesha wajasiriamali unaouwezo kwa kila mtu ambaye atakidhi vigezo
kukopeshwa kiasi cha Sh. milioni tano lakini pia serikali kupitia
shirika la NSSF na Sido wameingia makubalinaoa na benki ya Azania ili
kukopesha mtaji wajasiriamali kiasi cha Sh. miliini 50 hadi
100”amesisitiza

Hata hivyo amesema
kuwa serikali inaendelea kuwasilina na mamlaka husika katika maeneo
mbalimbali nchini ili kupata maeneo rasmi ambayo yatatengwa kwa ajili ya
wajasiriamali kufanya kushughuli zao.

Kwa upande wake Mkuu
wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amewataka wajasiriamali wa mkoa wa
Dodoma, kuwa wabunifu katika shughuli zao za kila siku ili kulikamata
soko la bidhaa zao.

“Msipokuwa makini
ujio wa makao makuu ya serikali nyinyi manaweza kuwa waangaliaji tu na
fursa zote wakachukua wageni hivyo basi mnapaswa kuvaa sura za kazi ili
mfikie malengo yenu kwa kubani zaidi bidhaa”amesema Mtaka

Awali Mlezi wa umoja
wa mafundi cherehani ambaye ni mbunge wa Dodoma mjini, Antony Mavunde
amesema kuwa tayari jiji la Dodoma limetenga ekari 8 kwa ajili ya
wajasiriamali ili waweze kukidhi mahitaji yao.

“Tumetenga kiasi
hicho cha eneo lakini pia na fedha ya kuanzia kiasi cha Sh. milioni 600
kwa ajili ya kuandaa eneo hili kwa ajili ya wajasirimali katika maeneo
ya Nzunguni jijini Dodoma”amesema Mavunde