Waziri
wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Leonard Chamuhiro,
akipatiwa maelezo na maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA), alipotembelea banda hilo mapema leo, baada ya ufunguzi wa
maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika leo na kesho katika
viwanja vya Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Maafisa wa BRELA kutoka
kushoto ni Afisa Usajili Bw. Englibert Barnabas, Msaidizi wa Usajili Bi.
Yvonne Massele na Afisa Leseni Bi. Saada Kilabula.
Maafisa
wa BRELA wakitoa elimu na huduma kwa watembeleaji wa Maonesho ya Wadau
wa Sekta ya Ujenzi yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar
es Salaam.
Afisa
Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bi. Saada
Kilabula ( aliyesimama kushoto) akitoa maelekezo ya huduma zitolewazo na
BRELA kwa Msanifu majengo Bw. E.Nnunduma, katika maonesho ya Wadau wa
Sekta ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,
tarehe 27 -28 Mei, 2021.
Afisa
Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.
Englibert Barnabas (kulia), akitoa ufafanuzi wa huduma zitolewazo na
BRELA kwa mteja kutoka Kampuni ya Agrovision Limited Bw. Arfaan Ahmed
Alwani, alipotembelea banda la BRELA, katika maonesho ya wadau wa Sekta
ya Ujenzi, yanayofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.