Na Mwandishi Wetu.
Leo Tarehe 18. Mei 2021 Naibu Katibu Mkuu (Sayansi), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe ametembelea Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam na kuongea na Menejimenti ya Taasisi hiyo kufahamu maendeleo na utekelezaji wa mradi wa EASTRIP ambao unatekelezwa DIT. Lengo kuu la mradi huo ni ujenzi wa Kituo cha Kikanda cha Umahiri wa Tehama (RAFIC).
Aidha katika mazungumzo hayo Dkt. Mdoe amepongeza mfumo wa ufundishaji unaotumiwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambao ni wa vitendo zaidi.
“DIT wana njia yao nzuri kwa kufundisha, wanafanya ufundishaji kwa vitendo zaidi, nawapongeza sana mnafanya vizuri lakini sasa mpeleke chini zaidi mafunzo yenu ili watu wengi wanufaike,” anasema Prof. Mdoe.
Prof. Mdoe katika ziara hiyo ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (Elimu na Ufundi Stadi), Prof. Caroline Nombo na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi, Dkt. Noel Mbonde.