Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Msuya akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Viwango
Afrika yatakayofanyika Mei 6 mwaka huu, Shirika la Viwango Tanzania
limeandaa zawadi kwa Wanafunzi 10 waliofanya vizuri katika uandishi wa
Insha ambapo mashindano hayo yalifanyika hivi karibuni katika Vyuo Vikuu
na Vyuo vya Kati hapa nchini.
Akizungumza na mwandishi wetu leo Jijini
Dar es Salaam, Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Msuya amesema kuwa katika
shindano hilo la Insha Mada Kuu ilikuwa ni UMUHIMU WA VIWANGO KATIKA
KUKUZA SANAA,UTAMADUNI NA TURATHI likiwa lengo kuwasaidia wanafunzi
wajue kwenye sekta husika ni nini kinahitajika katika kukidhi viwango.
“Tutawapa zawadi wanafunzi 10 walioshinda
shindano hilo pia watapelekwa kushiriki shindano la Afrika nzima
kumpata mshindi wa Afrika”.
Aidha Bw.Msuya amesema kuwa shindano hilo
liliandaliwa na Shirika la Viwango Afrikab(ARSO) ambapo TBS wao
walikuwa na jukumu la kusimamia hapa nchini.
“Ushiriki umekuwa mkubwa tumepata zaidi
ya wanafunzi 214 walioshiriki shindano hilo kutoka Vyuo Vikuu na Vyuo
vya Kati 32 hapa nchini”. Amesema Bw.Msuya.