Serikali yaahidi kumaliza changamoto zinazowakabili wamiliki wa mabasi nchini

 

Naibu
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara akifungua kikao wakati
alipokutana na Chama cha wamiliki wa Mabasi hapa nchini TABOA kwa lengo
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao
kilichofanyika leo May 3,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara akifungua kikao wakati
alipokutana na Chama cha wamiliki wa Mabasi hapa nchini TABOA kwa lengo
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao
kilichofanyika leo May 3,2021 jijini Dodoma.

Mjumbe wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) Elinas Kitua,akitoa
maoni wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara
pamoja na Chama cha wamiliki wa Mabasi hapa nchini TABOA kwa lengo
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao
kilichofanyika leo May 3,2021 jijini Dodoma.

Mmiliki wa Mabasi ya Arizona Coarch ,Yahaya Massare,akitoa kero zake
ambazo zinamkutana katika biashara zake za usafiri w Mabasi wakati
walipokutana na kikao ambacho kilikuwa lengo la kusikiliza kero
mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao kilichofanyika leo May
3,2021 jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) ambaye pia ni
Mmiliki wa Mabasi ya Isagilo Express kanda ya Ziwa Bw.Eliah
Peter,akizungumza kwenye kikao cha Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita
Waitara na Wamiliki wa Mabasi hapa nchini TABOA wenye lengo la
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao
kilichofanyika leo May 3,2021 jijini Dodoma.


Mmiliki wa Mabasi ya Super/Selons Express Francis Sengo,akizungumza
kwenye kikao cha Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe. Mwita Waitara na Wamiliki
wa Mabasi hapa nchini TABOA wenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali
zinazowakumba katika biashara zao kilichofanyika leo May 3,2021 jijini
Dodoma.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara ,akizungumza mara baada ya
kusikiliza kero za Wamiliki wa Mabasi hapa nchini TABOA Kikao ambacho
kilikuwa na lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazowakumba katika
biashara zao kilichofanyika leo May 3,2021 jijini Dodoma.



Baadhi ya washiriki wa Kikao wakimsikiliza Naibu Waziri wa uchukuzi
Mhe. Mwita Waitara(hayupo pichani) wakati ,akizungumza na Wamiliki wa
Mabasi hapa nchini TABOA Kikao ambacho kilikuwa na lengo la kusikiliza
kero mbalimbali zinazowakumba katika biashara zao kilichofanyika leo May
3,2021 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali
imewahakikishia chama cha wamiliki wa mabasi hapa nchini TABOA kuwa
itahakikisha inatatua na kumaliza changamoto zote ambazo ni kikwazo kwa
wafanyabiashara hao ikiwamo mfumo mpya wa ukatishaji tiketi mtandao.

Huku
ikizitaka taasisi zinazosimamia usafirishaji kuhakikisha wanatatua kero
na malalamiko yanayohusu wasafirishaji kwa wakati pindi zinapofika
ofisini kwao.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri
wa Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara alipokutana na chama cha wamiliki wa
mabasi hapa nchini TABOA kwa lengo kusikiliza kero mbalimbali
zinazowakumba katika biashara zao.

Ambapo amesema Serikali
inania nzuri ya kuhakikisha wafanyabiashara wa mabasi wanafanyakazi bila
ya kuwa na vikwazo kwani wao ni moja ya sekta muhimu ya kuchocheo
uchumi hapa nchini.

“Serikali inania nzuri sana na lengo lake ni
kuhakikisha ninyi mnafanyakazi kwa uhuru ndio maana leo nimekuja hapa
niwasikilize nini kikwazo kwenu kwa kuwa sekta yenu ni muhimu sana
kuwasafirisha wananchi ili nao walipe kodi nchi ijiendeshe” amesema
Waitara.

Ameongeza kuwa “Nimewasikiliza kero zenu zote
niwahakikishie tu kero zenu zote zitafanyiwa kazi hata hii kelele ya
muda mrefu ya tiketi mtandao tutalifanyia kazi kwa kuwa taarifa ni
kwamba mfumo unafanyiwa marekebisho bado haujawa rasmi utaboreshwa”
amesema.

Ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini LATRA
kuhakikisha kero, changamoto na malalamiko mbalimbali ya TABOA
yanafanyiwa kazi haraka pia wajenge utaratibu wa kusikiliza kero na
kuzijibu kwa wakati ili sekta ya usafirishaji iweze kukua hapa nchini.

“Nimepata
ushahidi hapa kwa barua mbalimbali kutokujibiwa na mimi mwenyewe
shahidi kuna taarifa yangu niliomba haijafanyiwa kazi pia kuna mbunge
mwenzangu katuma maombi ya kubadilisha tu rout(njia) lakini mpaka leo
haijajibiwa shida ni nini” amesema.

Aidha Mhe. Waitara amesema
atahakikisha anawakutanisha LATRA na TABOA ili malalamiko yao yote
yaweze kujibiwa moja kwa moja ili changamoto hizo ziweze kuondoka kabisa
sambamba na hilo ili LATRA waweze kuwapitisha katika mfumo huo ili
TABOA waweze kuelewa namna mfumo huo unavyofanyakazi na malengo ya
kuanzishwa kwake.

Awali wajumbe wa TABOA wameiomba serikali
kuitazama upya LATRA na muundo wake kwani kanuni zao nyingi si rafiki
kwao zinaweza kupelekea kupoteza mitaji yao kwa kufilisika kutokana na
makato mengi katika biashara hiyo.

Pia wamesema mfumo wa tiketi
mtandao wao ndio waanzilishi lakini sasa imekuwa tofauti na malengo ya
kuanzishwa kwake kwa sasa imekuwa mwiba kwao hasa baada ya kutakiwa
kujaza flot kabla ya kuanza kufanyakazi na kuwa na utitili wa makato
tofauti na mashine nyingine za kutolea lisiti.