Jamii yaaswa kutenga muda wa kukaa na watoto

 

Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya VUKA Initiative akifuatiwa na Katibu wa Taasisi hiyo Kabula Sukwa ,wa kwanza Julia Ni Mwinjilisti Wilson Kivuyo wa Kanisa la KKKT Usharika wa Oldonyosambu pamoja na Walezi wawatoto yatima walipokea msaada kutoka Taasisi hiyo,Mkurugenzi wa Taasisi ya VUKA Initiative  Vero Ignatus akizungumza na Walezi wawatoto Yatima katika Usharika wa Oldonyosambu uliopo Wilaya ya Arusha Dc Mkoa wa Arusha

Mkurugenzi wa Taasisi ya VUKA Initiative  Vero Ignatus akizungumza na Walezi wawatoto Yatima katika Usharika wa Oldonyosambu uliopo Wilaya ya Arusha Dc Mkoa wa Arusha

Katibu wa Taasisi ya VUKA Initiative Kabula Sukwa akizungumza na WALEZI wa watoto yatima katika Usharika wa Oldonyosambu wilaya ya Arusha DC Mkoani Arusha.

TENGENI  MUDA WA KUKAA NA  WATOTO TAMBUENI CHANGAMOTO ZAO

 Na.Mwandisi wetu Arusha

Jamii nchini
kuanzia ngazi ya familia wazazi na walezi,wametakiwa kuwa karibu na watoto, na
kufahamu changamoto mbalimbali wananzozipitia ikiwa ni sehemu ya mkakati wa
kudhibiti vitendo vya Ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia katika mazingira
wanayoishi.

Akizungumza katika jukwaa maalum la wadau wakutoa Elimu juu ya udhibiti wa masuala ya Ukatili wa Kijinsia, Mkurugenzi wa Vuka Initiative Vero Ignatus
alisema  wazazi wengi
wamesahau wajibu wao wa msingi,kwani mara nyingi wanadamka alfajiri kwaajili ya
shughuli za kujikimu kimaisha, na kuwasahau watoto na kuwatelekezea wasaidizi wa
kazi majumbani mwao.

Bi Vero alitoa rai kwa wazazi na walezi hao  kwa,mba pamoja na shughuli walizo nazo za kila siku za kujitafutia riziki, watenge muda kwaajili ya  kukaa na watoto wao pamoja na kuwafahamu zaidi.

Nae Kabula Sukwa ni Katibu wa VUKA, alisema kuwa Taasisi hiyo itagharamia mafunzo ya ujasiriamali kwa wajane zaidi ya 20 pamoja na kuchangia mifuko 50 ya saruji kwaajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha watoto yatima,kwani watoto hao bado wanalemewa na wasamaria wema na kuwa changamoto kubwa ya kukosa misaada hata kwa wafadhili.

Amewaomba wahisani wengine wajitokeze kungana pamoja na Taasisi ya VUKA  INITIATIVE ili kuhakikisha watoto hao yatima wanakuwa na kituo maalum cha kuwalelea tofauti na ilivyo sasa wanalelewa majumbami kwa wasamaria wema.

Akitaja changamoto wanazokutana nazo Mlezi wawatoto hao Mwinjilisti Wilson Kivuyo alisema kuwa Idadi ya watoto yatima Ni kubwa na nahitaji yao Ni mengi hivyo kwao imekuwa vigumu kwao kuwatosheleza kwa wakati mmoja ambapo baadi ya watoto hao wanasoma shule za msingi na sekondari na mahitaji yao ni mengi.

Aidha alitoa fursa kwa watu wenye huruma kushirikiana nao kuweka mikakati ya nguvu ya kuwasaidia yatima na wajane kwa mahitaji yao wakati wote,huku wakikusudia kuwaandalia semina ya faraja Mara 3 kwa kila mwaka .

Aidha taasisi hiyo ya Vuka Initiative iliweza kula chakula pamoja na watoto hao yatima 22,pia waliweza kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni ,mafuta ya kupaka,miswaki pamoja na kuchangia mifuko 50 ya saruji kwaajili ya kuanza ujenzi wa kituo cha watoto hao yatima.

Mwisho