Na
THABIT MADAI, ZANZIBAR.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza Uongozi
wa Mkoa Mjini Magharibi kuurejesha mnada uliokuwepo katika Soko la Mombasa
shimoni ambao umesimamishwa kwa takriban Mwaka Mmoja sasa.
Akishangiriwa
na Wafanyabiashara wa soko hilo kufuiatia kauli hiyo akiwa katika ziara ya
Wilaya ya Magharibi B katika mfululizo wa ziara zake kuangalia maendeleo na
chngamoto zilizomo katika Wilaya zote Mh. Hemed alisema Mkoa lazima
utafakari Mnada kwenye Masoko yote kwa kuzingatia mahitaji halisi.
Mh.
Hemed alisema kuanzia saa 24 zijazo akimaanisha asubuhi ya Jumatano mnada ndani
ya Soko hilo la Mombasa urejee kama kawaida ili kuwapa fursa Wananchi na hasa
Wafanyabiashara kupata huduma na riziki zao za halali.
Alifahamisha
kwamba si vyema Mwananchi akalazimishwa kufuata bidhaa muhimu za vyakula katika
masafa marefu wakati uwezo wa kufuata huduma hizo katyika masoko ya
karibu unawezekano endapo utapangwa utaratibu mzuri.
Mheshimiwa
Hemed alkitoa indhari kwa Wafanyabiashara kuendelea kufuata Sheria na taratibu
zilizowekwa kwa vile Serikali muda wote inapenda Wananchi wake
ambao nao kwa upande wao wana wajibu wa kuongeza ushirikiano wao kwa Serikali.
Kuhusu
Milango ya Biashara Mheshimkiwa Hemed alionya kwamba kitendo cha Mfanyabiashara
kupewa Mkataba wa kukodishwa Milango ya Biashara na baadae kumkodisha
Mfanyabiashara mwengine ni kuikosesha mapato Serikali Kuu. Aliutaka
Uongozi wa Baraza la Manispaa Magharibi B kuwajibika kwa kumpangisha Mlango yule
Mfanyabiashara wa Pili.
Alieleza
kwamba hatua hii inastahiki izingatie ile kodi ya ziada anayotoa mkodishwa
mwengine inaingia katika mfuko Mkuu wa Serikali badala ya fedha hizo kuendelea
kuingia mifukoni mwa wajanja na matapeli.
Mheshimiwa
Hemed alifahamisha kwamba wapo baadhi ya Wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya
kujilimbikizia milango mingi ya Biashara inayojengwa na kutolewa na Swerikali
na huamua kushirikiana na baadhi ya Watendaji wa Taasisi za Umma wasio
waadilifu tabia ambayo inapaswa kuonodhwa kwa kuopatiwa dawa ya kudumu.
Aliwaeleza
Wafanyabiashara hao wa Masoko ya Mombasa, Mwanakwerekwe na Jumbi kwa Serikali
Kuu kupitia Mabaraza ya Manispaa inaangalia mbinu muwafaka ya kujenga Soko
Kubwa na la Kisasa katika eneo la Wilaya ya Magharibi B kwa lengo lka
kuwaondoshea msongamano Wafanyabiashara wa Masoko hayo.
Akizungumzia
changamoto ya mafuriko ya Mvua za Masika zinazoathiri maeneo mengi ambayo
ujenzi wa Bara bara ilifanyika na kuathiri Makaazi ya Wananchi, Mh. Hemed
amewatahadharisha Wahandisi na Washauri Elekezi wanaosimamia Miradi kuwa
na hadhari na baadhi ya Wakandarasi wenye tabia ya kuodnosha njiani kazi
wanazopewa.
Mheshimiwa
Hemed alisema maeneo mengin yaliyopita Miundombinu ya Bara bara
yamekuwa na matatizo kadhaa yanayosababishwa na ukosefu wa Mitaro ya kupitishia
Maji machafu hasa wakati wa Kipindi cha Mvua kubwa za Masika.
Amewakumbusha
Viongozi wa Mikoa, Wilaya na wale wa Taasisi husika za Umma lazima wafanye
ziara za mara kwa mara kwa Wananchi tayari wameshajenga matumaini makubwa
juu ya uwajibikaji unaotekelezwa na Serikali yao.
Akilitembelea
eneo la Bwawa la Jiangamizini kwa Gizo la Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali
Mwinyi linalojaa maji ya Mvua hasa wakati wa msimu wa Masika makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman alisema Serikali itaunda Kamati
Maalum ya kufanya utafiti utakaobaini chanzo cha ongezeko la maji katika Bwawa
la Jangamizini.
Alisema
Kamati hiyo itakayoundwa na kutoa Ripoti yake ndani ya kipindi kifupi kijacho
itahusisha Wataalamu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Mamlaka ya
Mazingira, Ardhi, na baadhi ya Watu wanaoifahamu Historia na mwenendo halisi wa
Bwawa hilo.
Mapema
akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Serikali za Wilaya ya Magharibi B
hapo Ukumbi wa Halmashauri Mtaa wa Mombasa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Hamida
Khamis Mussa alisema vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikiongezeka siku hadi
siku.
Bibi
Hamida alisema ongezeko hilo linatokana na kasi ya Jamii kujitokeza kuripoti
matukio ya Vitendo hivyo vya udhalilishaji ambapo matukio 150 tayari
yameshafikishwa katyika Mamlaka husika ambayo ni polisi kwa hatua za kisheria.
Alieleza
kwamba Uongozi wa Wilaya kupitia Maafisa wake wa Ustawi wa Jamii imekuwa
ikiendelea kutoa Elimu ya jinsi Jamii inavyowajibika kushiriki kikamilifu
katika mapambano dhidi ya udhalilishaji hasa vile vya Ubakaji na Utelekezaji wa
Familia unaosababishwa na Wanandoa kutalikiana.
Akigusia
Migogoro ya Ardhi Bibi Hamida Khamis Mussa alibainisha kwamba uuzaji wa Viwanja
kiholela kwa Eka zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Kilimo nan a hata
Mashamba yanayorithiwa katika Familia ndio tatizo kubwa linaloleta
miogoro hiyo.
Alisema
malalamiko 105 ya Migogoro ya Ardhi hasa katika Jamii yameripotiwa na hadi sasa
67 imeshapatiwa Ufumbuzi wakati 38 ikiendelea na mchakato wa kutafutiwa suluhu
kwa kutumia Elimu kwa Wananchi juu ya kufuata Sheria pamoja na matumizi sahihi
ya Ardhi.
Katika
ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alibahatika kutembelea Jengo
jipya linalopjengwa la Mamlaka ya Chakula na Dawa, shughuli mbali mbali za
Vijana pamoja na Kituo cha Machinjio ya Nyama kiliopo Kisakasaka.