Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akizungumza kwenye kikao cha
Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara
yake kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma,kushoto kwake ni Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Exaud Kigahe (kulia) ni Katibu Mkuu wake Bw.
Dotto James.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akifafanua jambo wakati wa
kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini
ya Wizara yake kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe ,akieleza jambo wakati
wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara hiyo kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Dotto James akizungumza wakati
wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara hiyo kilichoongozwa na Waziri Prof,Kitila Mkumbo
kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil
Abdallah,akizungumza wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja
na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika April
10,2021 jijini Dodoma.
Sehemu
ya watumishi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.
Kitila Mkumbo (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara
pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika
April 10,2021 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ,amewataka watumishi wa
Wizara yake wote nchini kuimarisha sekta ya viwanda na biashara ili
kukuza uchumi nchini na kutekeleza malengo ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano
2021/22 – 2025/26.
Prof.Mkumbo
ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Menejimenti ya
Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo,amesema
kuwa majukumu ya wizara hiyo ni kutoa mwelekeo na utekelezaji wa kuinua
uchumi wetu.
Prof.Mkumbo
amesema kuwa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 ni kuona Tanzania
inahitimu na kuondoka kuwa nchi masikini inayotegemea kilimo na uchumi
wa uzalishaji duni na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo
Wizara ina mchango mkubwa katika kufanikisha azma hiyo.
“Uchambuzi
wa maudhui ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26 unaonesha wazi kabisa
nafasi ya Sekta ya Viwanda na Biashara,sisi kama Wizara tunatarajiwa
kutoa mchango karibu kwa kila eneo la matokeo tarajiwa.”
Aidha
amesema pia katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano
2021/22 – 2025/26, malengo sita kati ya mahsusi 12 yanahusu sekta ya
viwanda na biashara, kati ya vipaumbele vitano vya mpango huo vitatu
vinahusu wizara hiyo, katika Sekta 30 za mpango huo Sekta 6 zinahusu
Wizara na katika hatua 156 hatua 54 zinahusu Wizara ya Viwanda na
Biashara.
“Taasisi
zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zina mchango mkubwa katika
utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025 na Mpango wa taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano
2021/22 – 2025/26, Hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa
Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa
huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo”
Hata
hivyo, Prof.Mkumbo amesema kuwa hakusudii kutumia muda mwingi katika
kutunga Sera, Sheria na mikakati na kuwa yeye analenga katika
utekelezaji na kuona matokeo ya utekelezaji huo kwa kuchochea ukuaji wa
haraka wa Sekta ya Viwanda na Biashara.
Prof.Mkumbo
amewataka wataalamu wa Idara ya Sera na Mipango ya Wizara kusimamia
uhuishaji wa nyaraka mbalimbali za kisera na sheria ili ziende na
wakati na kuakisi maudhui ya Mpango wa tatu wa Maendeleo na maono ya
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Prof.Mkumbo amesema kuwa tunataka kuviendeleza viwanda hapa nchini
lazima kuwa na kanzi data ya kisasa ya viwanda kwa kuzingatia kiwango
cha uzalishaji na ajira, kuweka mazingira na masharti rahisi katika
kukuza na kuchochea viwanda vidogo vidogo vinavyotumia teknolojia rahisi
na ya kisasa na vilivyojikita vijijini na mijini,
Aidha
Waziri Mkumbo ameongeza kuwa lazima tuwawezeshe na kuwahudumia
wawekezaji katika viwanda vikubwa na vyenye tija katika uchumi na
kuhuisha Mkakati wa Viwanda nchini,ikiwemo dhana ya EPZ na SEZ.
Amesema
pia kusimamia kwa karibu miradi ya kielelezo iliyopo katika Mpango wa
Maendeleo wa Tatu wa Taifa ambayo ni mradi wa Chuma wa Mchuchuma na
Liganga, Magadi Soda wa Engaruka, ujenzi wa Kiwanda cha Sukari-Mkulazi
na kanda Maalum za Uchumi na Maeneo Maalum ya Uwekezaji
Prof.Mkumbo
amesema kuwa kuimarisha utafiti na matumizi yake katika maendeleo ya
viwanda, ikiwemo kuwa na ushirikiano wa karibu na taasisi za utafiti na
elimu ya juu na kupanua na kuboresha mahusiano na ushirikiano na taasisi
za sekta binafsi.
“Naomba tumeimarisha ushirikiano na OR-TAMISEMI katika maendeleo ya
viwanda vidogo vidogo, tunataka kuona uwezekano wa kuwaongeza majukumu
maafisa biashara wa Halmashauri ili pia wasimamie viwanda vidogo vidogo
katika maeneo yao kwa kushirikiana na SIDO.”amesema Prof.Mkumbo
“Tunataka tunapokutana na wafanyabiashara tufanye mazungumzo yenye tija
ya kubadilisha mikakati ya kukuza biashara na masoko, badala mikutano
hiyo kutumika tu kama jukwaa la kusikiliza malalamiko ya
wafanyabiashara.”
Pia naomba tuendelee kuzipitia kanuni za mamlaka za udhibiti
zinazoonekana kukwamisha biashara, kuchochea na kuhamasisha tabia ya
kujali wateja miongoni mwa watendaji wa Serikali wanaohudumia sekta
mbalimbali za biashara.
Aidha,
Prof. Mkumbo amesisitiza kuwa kuna haja ya watendaji wa wizara na
taasisi kubadilisha mtizamo katika utendaji kazi na kuwa na “corporate
thinking” na tabia ya kujali wateja kwa kuzingatia kuwa wadau
tunaowahudumia ni wafanyabiashara.
Waziri
Mkumbo amewataka wataalamu wa wizara hiyo kuhakikisha wanatoa ushauri
wa kitaalamu wenye ushahidi wa kisayansi na kuahidi kutoa ushirikiano
mkubwa kwa wafanyabiashara