Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi
wa NARCO na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kongwa wakati alipotembelea
Ranchi ya Kongwa kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akisaini kitabu cha
wageni wakati alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kabla ya
kuanza ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na wachungaji
wa ng’ombe (waliosimama kushoto) wanaomilikiwa na taasisi ya TALIRI
Mpwapwa wakati alipotembelea taasisi ya TALIRI na LITA Mpwapwa kwa lengo
la kukagua shughuli zinazofanyika. Waliosimama kulia ni Viongozi kutoka
Wizarani, TALIRI, LITA na Viongozi wa Wilaya ya Mpwapwa.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi
na watumishi wa TALIRI na LITA Mwapwapwa pamoja na viongozi wa Wilaya
wakati alipotembelea taasisi hizo kwa lengo la kukagua shughuli
zinazofanyika.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Mama Salma
Kikwete (wa kwanza kulia) katika duka la nyama kwenye Ranchi ya Kongwa
wakati alipotembelea Ranchi hiyo kukagua shughuli zinazofanyika.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Bw.
Mnyonaki (wa kwanza kushoto) ambaye ni mfugaji na mkulima wa malisho ya
Mifugo katika kijiji cha Msunjilile Wilayani Kongwa wakati
alipomtembelea kwa lengo la kuona shamba lake la malisho.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul (wa pili kutoka kushoto)
akiangalia eneo la kuchinjia kuku katika machinjio ya kuku iliyojengwa
katika kijiji cha Mbande Wilayani Kongwa wakati alipoitembelea Machinjio
hiyo.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ameitaka Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo Tanzania (TALIRI) kujiendesha kibiashara ili iweze kukabiliana
na changamoto zinazo ikabili.
Gekul
ameyasema hayo wakati alipo tembelea kituo cha TALIRI na LITA Mpwapwa
kwa lengo la kukagua kazi zinazofanywa na taasisi hizo.
Katika
taarifa iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TALIRI, Dkt. Jonas Kizima
ilielezea changamoto wanazokabiliana nazo zikiwemo za upungufu wa
watumishi, uhaba wa vitendea kazi na uhaba wa rasilimali fedha kwa
shughuli za kiutafiti. Lakini pia alizungumzia mikakati waliyonayo
katika kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa
kuwa changamoto nyingi zinahitaji fedha ili kuzitatua ndipo Naibu
Waziri Gekul akawaagiza TALIRI kujipanga vizuri ili sasa waweze
kujiendesha kibiashara kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutatua
changamoto walizonazo badala ya kusubiri kupata fedha kutoka Serikalini.
Pia
amewapa miezi mitatu kuhakikisha wanawalipa vibarua wanaochunga ng’ombe
pamoja na walinzi mishahara yao ya miezi sita wanayodai.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri amemshukuru Naibu Waziri
kwa maamuzi yake ya kitembelea taasisi hizo na kutatua tatizo la
mishahara ya vibarua na walinzi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Bw. Jonas Kizima amesema wamepokea maelekezo
yaliyotolewa na Naibu Waziri na watakwenda kuyafanyia kazi hasa suala
la taasisi hiyo kujiendesha kibiashara.
Katika
ziara yake hiyo Wilayani Mpwapwa, pia ametembelea wilaya ya Kongwa
ambapo amatembelea Ranchi ya Kongwa, shamba la malisho la mfugaji Bw.
Mnyonaki lililopo katika kijiji cha Msunjilile wilayani Kongwa na
Machinjio ya kuku iliyopo katika kijiji cha