Sekta ya uvuvi yafanikiwa kupunguza biashara haramu ya mazao ya uvuvi kwa asilimia 80

 

Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza wakati akifungua 
mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi katika ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo mjini Dar es Salaam. Wadau
wa sekta ya Uvuvi wakifuatilia mkutano wa wadau hao katika ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo mjini Dar es Salaam. Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika
mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi katika ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo mjini Dar es Salaam.

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza katika katika
mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi katika ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo mjini Dar es Salaam.

Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda akizungumza katika katika mkutano
wa wadau wa sekta ya uvuvi katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere leo mjini Dar es Salaam.


Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki akipata picha ya pamoja na wadau
mbalimbwa wa sekta ya uvuvi katika mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi
katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo mjini Dar
es Salaam.



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Sekta ya Uvuvi imefanikiwa
kupunguza uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi kwa asilimia 80 kwa
upande wa maji baridi na asilimia 100 kwa matumizi ya vilipuzi katika
Ukanda wa Bahari ya Hindi. 


Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki ameyasema hayo leo wakati akifungua  mkutano wa wadau wa
sekta ya uvuvi wa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere mjini Dar es salaam.


Aidha Mhe.Ndaki amesema
Serikali inatarajia kuanza utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo
na Uvuvi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Kuendeleza Kilimo
(IFAD). Programu hiyo imelenga kununua meli nane (8) zitakazokabidhiwa
kwa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) meli nne (4) na Kampuni ya Uvuvi
ya Zanzibar (ZAFICO) meli nne (4).


Amesema serikali inaendelea na
mpango wa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo kazi
mbalimbali zimefanyika ikiwemo uandaaji wa Mpango Biashara (Business
Plan) wenye maeneo matatu makubwa. Maeneo hayo ni uvuvi wa bahari kuu,
ufugaji samaki na uchakataji wa mazao ya uvuvi.


Pamoja na hayo Mhe.Ndaki
ametoa wito kwa wadau kutumia fursa ya mkutano huo kuainisha changamoto
zinazoikabili sekta hiyo kuanzia ngazi ya mvuvi mmoja mmoja, Vyama vya
Wavuvi, Wachakataji wa samaki na mazao yake, Serikali na Washirika wa
Maendeleo.


“Tumieni jukwaa hili
kuzijadili changamoto hizo na kisha kuwasilisha Wizarani mapendekezo ya
namna bora ya kuzipatia ufumbuzi. Vilevile, ainisheni wahusika na muda
wa utatuzi wa changamoto hizo kwa kuzingatia kuwa zipo changamoto ambazo
utatuzi wake ni wa muda mfupi, wa kati na mrefu”. Amesema Mhe.Ndaki.


Hata hivyo Mhe.Ndaki amesema
kuwa katika mwaka 2020, jumla ya tani 497,567 za samaki zenye thamani ya
shilingi trilioni 2.34 zilivunwa ikilinganishwa na tani 362,645 zenye
thamani ya trilioni 1.48 mwaka 2015/2016. Kati ya tani hizo, tani
435,408.9 ni kutoka maji baridi na tani 62,158.38 zilitoka maji chumvi
mwaka  2020 ikilinganishwa na tani 409,332.72 zilizovunwa kutoka maji
baridi na tani 60,976.51 kutoka maji chumvi mwaka 2019. Ongezeko la
uvunaji wa rasilimali za uvuvi umetokana na kupungua kwa vitendo vya
uvuvi haramu hali iliyosababisha kuongezeka kwa samaki katika maji yetu.


Kwa upande wake Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul amesema kuwa katika mkutano huo
watajadili mambo mengi yanayohusiana na sekta ya uvuvi na kuona ni
changamoto gani wananzipitia na kisha kuzitatua ili kuweza kukuza sekta
hiyo.


Aidha Mhe.Gekul amesema mpaka
sasa zaidi ya watu milioni 4.5 wanajihusisha na sekta ya uvuvi ambapo
wanategemea kuongeza ajira zaidi ya elfu 30 katika sekta hiyo.


“Tutaangalia na kujadili
vikwazo ambavyo wanapitia kwenye viwanda vyetu na kuona viwanda hivyo
vinaweza kuendelea na kuongeza ajira ambapo mpaka sasa tuna viwanda 14
katika sekta hii vinafanya kazi ikiwa 9 kule Ziwa Victoria na 5 katika
ukanda wa bahari, hivi vinatosha  na kuchakata mazao yanayotokana na
uvuvi”. Amesema Mhe.Gekul.