Katibu tawala wa wilaya ya rungwe afurahishwa na juhudi zinazofanywa na tbs

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Bw.
Mnkondo Bendera amelipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa
jitihada inazozifanya za kuwafikia wajasiriamali na wananchi kwa ujumla
na kuwapatia elimu ya viwango na uthibitishwaji wa ubora wa bidhaa.
Elimu hiyo itawawezesha kuzalisha bidhaa kwa kufuata viwango na zenye
ubora na na hivyo basi wateja wao kutumia bidhaa bora na salama sambamba
na thamani ya fedha wanazotumia kununulia bidhaa hizo.

Bw. Bendera ametoa pongezi hizo mapema
leo alipotembelewa na maafisa kutoka TBS na Wizara ya Viwanda na
Biashara wakiongozwa na Meneja Mafunzo na Utafiti Bw. Hamisi Sudi
walipofika ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kuanza mafunzo kwa
wajasiriamali wanaozalisha na kuuza mafuta ya kula wilayani hapa.

Wakati huo huo, Bw. Bendera ameliomba
shirika kupanua wigo wa mafunzo ili yawafikie wauzaji wa vyakula maarufu
kwa jina la mama na baba lishe (Mama na baba ntilie).Bw.Bendera amesema
baba na Mama lishe walio wengi wamekuwa wakipika na kuuza chakula mara
nyingi ugali na wali na kuufunika au kufungasha katika mifuko ya nylon
(plastics) jambo ambalo linahatarisha usalama wa afya za walaji.

Akilitolea maelezo kuhusu maombi hayo
Meneja Sudi alisema Shirika kwa sasa liko katika hatua ya kukamilisha
kanuni na taratibu zitakazotumika kuwashirikisha Maofisa wa TAMISEMI
.Maofisa hao wanajumuisha Maofisa afya,Biashara na Ustawi wa jamii
katika ngazi za halmashauri ili waweze kuwafuatilia kwa karibu na
kuwapatia elimu juu ya uaandaji na uhifadhi bora na salama wa chakula.

Aliongeza kuwa tangu mwezi Julai,2019
TBS imeongezewa majukumu yanayotokana na Sheria ya Fedha Na.8 ya Mwaka
2019,ambapo majukumu ya usajili wa bidhaa za Chakula ,Vipodozi na
majengo yanayoendeshea Biashara ya bidhaa hizo, yamehamishiwa TBS kutok