Dkt.chaula alitaka shirika la posta nchini kufanya kazi kwa weledi

 

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab
Chaula akizungumza wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la
wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini
Dodoma.



Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim
Yonazi ,akizungumza wakati wa kufunga kikao cha baraza la 27 la
wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini
Dodoma.



Posta
masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe,akielezea
jinsi walivyojifunza mafunzo hayo kwa siku tatu wakati wa kufunga kikao
cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini
kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.




Baadhi
ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati
akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta
nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma


Katibu
Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula
amelitaka baraza la wafanyakazi wa shirika la posta Tanzania kufanyakazi
kwa weledi na kuweka mikakati ya kuhakikisha shirika hilo linajiendesha
kwa faida na kuchangia uchumi wa taifa.


Dkt
Chaula ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha baraza la
27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini waliokutana kujadili na
kutathmini utendaji kazi wa shirika hilo katika utendaji kazi wake.


Amesema
ni wajibu wa kila mtumishi ndani ya shirika hilo kuhakikisha
anafanyakazi kwa bidii na kuongeza tija katika shirika na kuongeza
uzalishaji kama ilivyokusudiwa wakati wa uanzishwaji wa shirika hilo.


“Kila
mtu ndani ya shirika ajitathmini amelifanyia nini shirika, kila taasisi
imewekewa target ataongeza vipi ajira mpya za ndani kama nchi
tumejiwekea ajira milioni nane 8,000,000 kati ya hizo je taasisi yako
itatoa ngapi” amesema Dkt Zainabu Chaula.


Aidha
Dkt.Chaula amelitaka shirika kujitathmini katika utendaji kazi wao
katika Mkoa yote kuhakikisha Mikoa yote inafanya vizuri na kusaidia
Mikoa ambayo haifanyi kazi vizuri ili nayo ifanye kazi vizuri.


Dkt.Chaula
amesema kuwa kwa sasa utendaji kazi wa shirika unazidi kuimarika hivyo
kila mtumishi kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kuendelea
kuboresha zaidi huduma zinazotolewa na shirika la posta.


Aidha
amewataka wajumbe wa baraza kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata juu
ya huduma mpya zilizoanzishwa na shirika na kuongeza mchango katika
kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya mawasiliano.


Awali
Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe amesema
baraza limekaa kwa siku tatu (3) likishirikisha watumishi kutoka ngazi
mbalimbali kwa lengo la kutathmini na kuweka malengo katika kuimarisha
utendaji kazi wa shirika la posta.


Aidha
katika siku tatu hizo walipata wasaa wa kuchagua viongozi mbali mbali
wa baraza na kupata mafunzo ya viashiria vya hatari katika uzalishaji wa
shirika na kukuza uchumi wa nchi na utunzaji wa nyaraka za shirika.