Watalii wanaofika nchini hutegemea taarifa za vyombo vya habari

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Nzuki

Wizara ya  vya habari vyaombwa kujenga taswira nzuri ya Taifa Kuvutia watalii.

Mussa Juma, APC Media

Ngorongoro.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dk Aloyce Nzuki ameviomba vyombo vya habari nchini kujenga taswira nzuri kwa Taifa ili kuvutia watalii.

Akifungua Warsha ya wahariri na Waandishi wa habari waandamizi wa habari za Maliasili na Utalii,leo Desemba 28 Ngorongoro amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa kusaidia kukuza Utalii nchini.

Amesema wanahabari wanapaswa kujenga taswira nzuri kwa watalii kabla ya kufika nchini,wakiwa nchini na baada ya kuondoka nchini.

Dk Nzuki amesema lengo la serikali ni kufikia watalii millioni 5 mwaka 2025 na kuingiza mapato dola 6 bilioni na hayo yatawezekana kamanvyombo vya habari vikiunga mkono jitihada za serikali.

Amesema kwa sasa asilimia 70 ya watalii wanaokuja nchini hupata taarifa Kwa kuisikia vizuri Tanzania.

Hata hivyo amesema kuna Changamoto kwani asilimia 80 ya watalii waofika nchini kila mwaka ni wapya na ni asilimia 20 Tu ndio wanarudi.

Akizungumzia mikakati ya kuongeza watalii amesema serikali inataendelea kuongeza utangazaji Utalii,kuboresha huduma kwa watalii na kutoa elimu kwa watoa huduma za Utalii.