WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu
katikati akizungumza leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa TRA mkoa
wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao hicho
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU
wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa kikao hicho
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mstahiki Meya
wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo
KATIBU wa JWT Mkoa wa Tanga Ismail Masoud akizungumza jambo kwenye kikao hicho
AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akieleza jambo kwenye kikao hicho
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akieleza jambo kwenye kikao hicho
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbaliWadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Mkoa wa Tanga wasichoke kutoa elimu ya mlipa kodi kutokana na kwamba kodi ndio
msingi na uhai wa maendeleo ya Taifa.
Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Tanga(CCM) aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa
TRA Mkoa wa Tanga kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
ambapo alisema suala la elimu kwa walipa kodi ni muhimu ili waweze kutambua
umuhimu wake.
Alisema suala la utoaji wa elimu ni muhimu sana na
iendelee kutolewa kwa kila mtu yupo tayari kulipa kodi na tupo kutokana na
maendeleo lakini kikubwa waendeele kutoa elimu ambayo itakuwa ni chachu kubwa
ya kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya ukusanyaji wa kodi.
“Ndugu zangu TRA mnafanya kazi kubwa
na nzuri lakini msichoke endelee kutoa elimu na wanatambue umuhimu wa kulipa
kodi kwa sababu msipotoa elimu kuna watu wanaingia kwenye gharama kubwa zaidi
kutokana na ujanja ujanga na kwa sababu hawana elimu ndio wanakwepa kulipa kodi”Alisema
“Lakini pia kuna baadhi ya watumishi
sio waaminifu kesho anakwenda anachukua elfu ishirini na siku inayofuatia elfu 50
jamani tubadilike tuachane na masuala hayo lazima tusisitze umuhimu wa kulipa
kodi kwa wafanyabiashara “Alisema
Akizungumzia masuala ya makadirio,
Waziri Ummy aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha wanatenda haki kwa kuangalia
uhalisia wa biashara au huduma inayotolewa kwa sababu unaweza kumpa mtu
makadirio ya bei ya juu badala ya kumsaidia ukidhani kwamba ndio utapata kodi
kumbe hupati.
“Mkiwapa kodi ambayo ni halali
watajua ni wajibu wao na wataweza lakini niwaambie kwamba Serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Dkt John Magufuli inawapenda walipa kodi na wafanyabiashara
na nihimize kuhakikisha mnalipa kodi”Alisema
Awali akizungumza wakati akifungua
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema ulipaji wa kodi ndio
ute wa mgongo wa Taifa lolote hivyo hawana budi kujipanga vizuri kuhakikisha
watumishi wa TRA na wafanyabiashara hawajengeani mazingira ya chuki
Alisema mazingira hayo yanatokana na
wao kudhani watu wa TRA wanakuja na makadirio yasikuwa na utaratibu hivyo
aliwataka kuhakikisha wanafanya biashara kwa uwazi na watoe ushirikianokwa TRA na TRA wahakikishe wanaendesha shughuli
zao kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma.
Awali akizungumza katika kikao hicho
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Specioza Owure alisema kwamba hivi sasa
watawakamata watu wasiodai risiti huku akieleza kwamba kampeni hiyo wanataka
kuanzisha wakati wowote ule.
Akizungumzia lengo lao la ukusanyaji
wa mapato kwa mwaka 2020/2021ambapo alisema kwa upande wa Idara za kodi za
ndani inalengo la kukusanya Bilioni 66 na mpaka sasa wana asilimia 120 ya hilo
lengo huku kodi za Forodha ikiwa ni bilioni 66 na asilimia 83 lakini kimkoa
lengo kuu kukusanya Bilioni 138.9 hivyo wan kazi kubwa ya kufanya