Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la polisi mkoa wa Arusha,linawashikilia watu tisa wakiwemo askari watatu wa jeshi la polisi makao makuu Dodoma na mkoa wa kipolisi Kinondoni, kwa kujihusisha kushawishi na kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa madini jijini Arusha
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni D/C mwenye namb G 5134 Heavenlight Mushi, Idara ya Intelijensia mkoa wa Kinondoni, H 1021 PC Bryton Murumbe askari kazi za kawaida mkoa wa Dodoma,H 125 Gaspal Paulo, Idara ya Intelijensia makao makuu Dodoma.
Wengine ambao ni raia amewataja kuwa ni Shaban Bensoni miaka 40 mfanabiashara na mkazi wa Makole Dodoma, Joseph Damiani Chacha miaka 43 mfanabiashara mkazi wa Ilboru jijini Arusha, Omary Alphonce Mario miaka 43 mfanyabiashara mkazi wa Olerien jijini Arusha, Lucas Michael Mdeme, miaka 46 mfanyabiashara,mkazi wa Engutoto, jijini Arusha na Nelson Lyimo,miaka 58 mfanyabiashara mkazi wa Kimandolu,jijini Arusha na Leonia Joseph miaka 40 Sekretari wa kampuni hiyo a madini ambae ni mkazi wa Ilboru,
Amesema uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea na jalada limepelekwa kwa ofisi a mwendesha mashitaka na kwa upande wa askari hao wanaoyuhumiwa taratibu za kijeshi zinaendelea.
Aidha amesema kuwa watuhumiwa hao ambao ni askari walimfuata mfanyabiashara wa madini kampuni a Germs and Rock s Ventures iliyopo mtaa wa Pangani jijini Arusha, na kupokea kiasi cha shilingi milioni 10 na walikuwa wamefuata kiasi cha shilingi milioni 20 zilizokuwa zimebakia.
Amesema kuwa askari hao walienda kumtishia mfanyabiashara huyo na kudai kuwa alikuwa hana vibali va kufana biashara a madini, ndipo polisi walipotaarifiwa na kuwakamata watuhumiwa hao ambao walishirikiana na raia .