Mbunge ummy mwalimu ataka umoja na mshikamano madiwani wa jiji la tanga

 

 
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya
Meya wa Jiji la Tanga
Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo
Meza
kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uchaguzi huo katikati ni
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia ni Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge  na kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza na waheshimiwa madiwani kabla ya kuanza uchaguzi huo
Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akiwa na Mstahiki Meya mpya
wa Jijini la Tanga (CCM) Abdurahaman Shillow kushoto na anayefuatia ni
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi
Mwanaisha Ulenge
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu
amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji
la Tanga ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Jiji la Tanga.

Mhe
Ummy ameyasema hayo leo katika kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya
Meya wa Jiji la Tanga ambapo ameeleza  kuwa uchaguzi umekwisha na
wananchi wa Tanga Mjini wamewaamini  kwa kuwapa ushindi mkubwa kwa
mgombea Urais, Ubunge na Madiwani wa CCM katika kata zote 27 za Tanga
Mjini.
 
Alisema baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi hao wana wajibu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga mjini bila
kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Mhe
Ummy amempongeza Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow kwa kuaminiwa kuwa Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga huku akihaidi kumpa ushirikiano wakati wote wa
utekelezaji wa majukumu yake.

Katika
uchaguzi huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa
Tanga ulisimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
 
Akitangaza
matokeo hayo Mwilapwa alimtangaza Mhe Abdurahmani Shillow ambaye ni
Diwani wa  Kata ya Mzingani ambaye ni  mgombea Umeya wa Jiji la Tanga
kwa kupata kura 26 huku nafasi ya pili ikienda kwa  Mhe Said Mbaruku
ambae amepata kura 11 wakati Mhe Ahmed Mwinjanga amepata
kura 1 katika idadi ya  wapigakura walikuwa 38.