Bunge la Peru limepiga kura ya kumuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo, Martin Vizcarra (57) kufuatia tuhuma za ufisadi. Jumla ya Wabunge 105 kati ya 130 walipiga kura ya kumvua Uongozi
Akizungumza baada ya mchakato huo Vizcarra ambaye amekana tuhuma zinazomkabili amesema amekubali matokeo, hatochukua maamuzi yoyote ya kisheria, atatoka Ikulu na kwenda nyumbani
Spika wa Bunge, Manuel Merino anatarajia kuongoza nchi hiyo hadi Julai 2021 ambapo muhula wa Rais huyo aliyeongoza tangu mwaka 2018 ungemalizika.