MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah amewataa wananchi wa wilaya hiyo kujikita zaidi katika maandamano ya shambani na katika shughuli za kimaendeleo badala ya kuwasikiliza waliokuwa wagombea wa nafasi mbali mbali wanaowaza kuvuruga amani kwa kutamani maandamano yasiyo na tija ya kiuchumi .Mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa
Akizungumza jana na kituo cha matukio daima Tv mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa muda wa kampeni kwa ajili ya kupata viongozi watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano umekwisha pita na sasa ni wakati wa wananchi pamoja na viongozi hao kufanya kazi .
Hivyo alisema itakuwa si sawa kwa mwananchi wa Kilolo kuacha kufanya shughuli za kimaendeleo na kushughulishwa na maandamano yasiyo na tija katika ustawi wa maisha yao .
” Tunahitaji kuona wanasiasa sasa wanashiriki katika ujenzi wa Taifa kwa kuhamasisha wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo kuliko kuhamasisha wananchi kwenda barabarani kuandamana”
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana wilaya ya kilolo kuwapuuza wale wote ambao wanatamani kuona amani ya nchi hii inavurugwa kwa kutamani maandamano na vurugu badala yake anatamani kuona kila kijana anajishughulisha katika kazi za uzalishaji mali .
Asia alisema katika wilaya ya Kilolo uchaguzi umefanyika katika hali ya amani na utulivu mkubwa na kuwapongeza wananchi kwa kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa amani na utulivu pia kuwapongeza wale ambao wamechaguliwa kuwa viongozi akiwemo Rais Dkt John Magufuli ,mbunge wa kilolo Justin Nyamoga na madiwani wote waliochaguliwa .
Aidha aliwataka wazazi wilayani humo kuendelea na maandalizi ya kuwapeleka watoto wao shule hapo mwakani .
Kwani alisema ni jukumu la kila mzazi ama mlezi kuhakikisha mtoto wake anapata elimu na anasimamiwa vema ili kupata elimu hiyo mwanzo hadi mwisho bila kukatishwa masomo ama mzazi kumgeuza mtoto huyo kuwa ni sehemu ya watafutaji wa fedha za familia .
Alisema kwa wale watoto waliohitimu elimu ya msingi wazazi kuendelea kuwalea kwa kuwalinda watoto hao ili wasirubuniwe na mtu yeyote kwenda mijini kufanya kazi za ndani ama kupewa mimba kwa wale wa kike.
” Serikali hii chini ya Rais Dkt John Magufuli imeendelea kuboresha mazingira bora ya elimu kwa kuondoa changamoto mbali mbali katika elimu hata kuamua kufuta ada kwa elimu msingi ” alisema
Hivyo alisema jukumu la mzazi na mlezi ni kusimamia watoto kwenda shule na kuwalinda na vikwazo ambazo vinaweza kuwavurugia masomo yao na sio wasimamizi hao wa mtoto kuwa chanzo cha kuwaharibia maisha watoto hao kutofikia ndoto za serikali za elimu bora.
Asia alisema serikali haitaacha kuwachukulia hatua wazazi ama walezi ambao watabainika kuwakwamisha watoto wanaopaswa kwenda sekondari ama kupata elimu .
Kuhusu