Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba (MB) akizungumza na Watumishi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi
Kaali akimweleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba utekelezaji
wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka 2020 hadi 2025
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi
Kaali akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba (MB) katika
Ofisi za Tume jijini Dodoma. Wakati wa ziara yake ya kuwatembelea na
kuzungumza na watumishi wa Tume Makao Makuu na Watumishi wa Tume mkoa wa
Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka watumishi wa
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu kufanya kazi kwa bidii na weledi ili
kutimiza azma ya serikali kusogeza huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo miundombinu
bora ya umwagiliaji kwa wakulima
Mgumba aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya kutembelea na
kuzungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu na
Watumishi wa Mkoa wa Dodoma alisema suala hilo ni muhimu kwa wakulima hatua
ambayo itawawesha kuinua vipato vyao na Taifa kwa ujumla.
Alisema pia kuhakikisha wanakuwa tayari kwa jukumu kubwa la
kujenga na kusimamia miradi ili iweze kuleta tija kwa maendeleo ya wakulima na
jamii nzima
“Kwa kweli niwapongeze watumishi wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji kwa kupata hati safi na lakini niwatake muendelee kufanya kazi kwa
bidii na weledi”Alisema
Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, akimweleza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba
utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka 2020 hadi
2025 kwa kueleza imejipanga kutekeleza mipango ya serikali ya kukarabati na
kujenga Skimu Mpya.
Alisema pia mipango mengine ni kuratibu mipango ya tozo
katika Skimu za Umwagiliaji sanjari na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na
kuhakikisha nchi inavuka kiwango cha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara
kutoka asilimia 24 za sasa hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 ambapo
pia eneo la Umwagiliaji litaongezwa kutoka Hekta 694,715 hadi Hekta 1,200,000.